ANGALIA LIVE NEWS

Friday, June 20, 2014

WATU WATATU WAJERUHIWA KWA RISASI ZA MOTO BAADA YA KUKUTWA WAKICHEZA NGOMA ZA VIGODORO BILA NGUO



Watu watatu wakazi wa Mwananyamala Jijini Dar Es Salaam wamejeruhiwa katika tukio lililohusisha risasi za moto linalodaiwa kufanywa na polisi baada ya kukutwa wakikesha kwenye ngoma maarufu za Kigodoro, ambazo tayari zimekwishapigwa marufuku na jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam.
 
Tukio hilo lilitokea majira ya saa kumi na nusu jioni katika eneo la shule ya msingi kisiwani ambapo mmoja  wa  majeruhi hao  tayari amekwisahruhusiwa kurudi nyumbani na mwingine akiendelea na matibabu kwenye hospitali ya Mwananyamala.
 
Wakiwa kwenye ngoma hiyo maarufu Jijini Dar es Salaam ya Kigodoro, eneo la Kisiwani mwananyamala, mara gahfala polisi walivamia eneo hilo, na kusimamisha shughuli nzima kwa madai ya kucheza wakiwa hawana nguo, jambo ambalo ni kinyume na maadili.
 

Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa kipolisi Kinondoni Kamishna msaidizi Camillius Wambura anathibitisha kutokea kwa tukio hilo.

2 comments:

Anonymous said...

Huu ni uonevu mtupu, kwanini unatumia ri sasi za moto wakati hakuna Mtu anayehatarisha maisha ya m wingine.hawawagusi MAFISADI ambao hufanya maisha ya wananchi kuwa .lakini ni wepesi sana kuona mabaya ya wananchi.nasema dawa yao ipo inachemka.dj bana na hii.

Anonymous said...

Huo ni ugaidi uliokithiriiii! Kwanini muwapige kwa risasii za moto? Wameiba? Wameua? Wamemjeruhi mtu? Ku mpiga mtu risasi za moto Kisa kucheza Ngoma ni ugaidi kabisaa! Mmekazana kuwashika al khaida na Wengine kumbe police wenyewe ndo magaidi!!!! Haki IKo waapi jamani? Watanzania tuna mwagana damu wenyewe kwa wenyewe?? Very sad! Siaminiiii!