Advertisements

Saturday, July 26, 2014

AJALI YA GARI YA WALIYOIPATA WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI AKIWEMO BAHATI BUKUKU


Gari lenye namba IT 7945 Toyota Nadia likiendeshwa na EDSON MWAKABUNGU (31) mkazi wa Tabata Dar es Salaam liliacha njia na kugonga gema na kusababisha majeraha kwa watu watatu baada ya kugongwa na gari jingine linalosadikiwa kuwa Fuso.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi David Misime SACP amesema ajali hiyo imetokea tarehe 26.07.2014 saa tisa alfajiri katika barabara kuu ya Morogoro – Dodoma eneo la Ranch ya NARCO Wilaya ya Kongwa.

Waliojeruhiwa ni EDSON MWAKABUNGU ambae analalamika maumivu sehemu za vidole vya miguu yote, BAHATI BUKUKU (40) ambae ni mwimbaji wa nyimbo za injili na mkazi wa Tabata – Dar es Salaam ambaye analalamika maumivu sehemu mbalimbali za mwili wake.

Mwingine ni FRANK CHRISTOPHER (20) mwimbaji pia wa nyimbo za injili mkazi wa Tabata Dar es Salaam ambapo kapata michubuko usoni na mkono wa kulia.

Wote wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kongwa kwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri ambapo Kamanda Misime amesema walikuwa wanatokea Dar es Salaam ambapo dereva alikuwa anelekea DRC – Kongo, BAHATI d/o BUKUKU na FRANK s/o CHRISTOPHER walikuwa wanakwenda Kahama kwenye tamasha la Injili.

Uchunguzi wa ajali hii unaendelea ikiwa ni pamoja na kutafuta gari lililowagonga.
CREDIT:MILLARD AYO

No comments: