ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, July 27, 2014

BAADA YA OMMY DIMPOZ KUONGELEA UPUNGUFU WA VIFAA KWA DIRECTORS.

Baada ya Ommy Dimpoz kuongelea upungufu wa vifaa kwa directors: Nisher adai wasanii wanadharau

Siku moja baada ya msanii wa muziki wa bongo fleva Ommy Dimpoz kutoa maoni yake juu ya sababu za wasanii wengi akiwemo yeye mwenyewe kufanya shooting za video zao nje ya Tanzania na directors wa nje, Directoe Nisher ametoa yake ya moyoni kwa kudai wasanii wanadharau directors wa bongo na kudai kutowahi kulipwa zaidi ya milioni 4 na msanii tangu alipoanza kufanya kazi hiyo licha ya kutengeneza video kali
Comment hiyo ya nisher kupitia ukurasa wake wa insta umeonyesha wazi kuwa ni majibu ya kile alichokisema Dimpoz kuwa directors inabidi wajiweke sawa kwenye upande wa vifaa maana ndicho kinachowakimbiza kwenda ncje ya Tanzania 

Hiki ndicho alichokizungumza OMmy Dimpoz
"biashara ya video ishaingia ushindani kwahiyo kuna haja ya kuwekeza kwenye vifaa, mi nauhakika mtu anamavifaa kibao anaenda kushoot lushoto huko noma, wazungu wenye watauliza umeshoot wapi, tuna maeneo kibao zanzibar wapi wapi wapi ya kushutia, sio kwamba hatun amaeneo, maeneo tunayo lakini hatujawa na vile vitu.kwahiyo nado maana hata mtu unafikiria sijui nishutia zanzibar lakini unawaza kumchukua labda God Father kumleta huku Tanzania ndio mziki. Halafu mtu utakapoletea vifaa hivyo nauhakika hautaishia kwenye video tu, kuna matangazo, utakodi utafanyaje, kuliko wanatoka watu nchi za watu makampuni yanalipa dola laki tatu kushoot tangaza wakati watu tungekuwa na vifaa., watu lazima waelewa kitu kimoja, hakuna mtu anaependa kujitia gharama kama kuna uwezo wa kuepuka ghara, sio ufahari, mi nnavitu vingi vya kufanya sio kwamba nataka tu nikalipe dola elfu 30 kushoot video wakati ninauwezo wa kuokuoa hiyo hela labda kulipa dola elfu 15 au 10 wadau wanatuskia sie ndo wasanii wenyewe tunasema kuwa mziki sasa hivi unalipa, mnaona sasa hivi vijana wenu wanapata shilingi mbili tatu hizo mbili tatu mtagawana nao vipi kuliko kwenda kuwapa watu wengine huko nje ya nchi? "

No comments: