Advertisements

Wednesday, July 23, 2014

CADAVER: MAITI ZINAZOTUMIWA NA WANAFUNZI WA SAYANSI YA TIBA


Mwaka 335-280 nchini Ugiriki kabla ya kuzaliwa kwa Kristo alitokea mwanasayansi nchini humo aitwaye Herophilus, huyu ndiye mtu wa kwanza kujenga mafunzo juu ya maumbile ya mwanadamu, kitaalamu 'Anatomy'Mwanasayansi huyu ndiye baba wa somo la Anatomy yaani maumbile ya mwili. Huyu ndiye aliyebainisha kuwa ndani ya mwili wa mwanadamu kuna damu na si hewa. Kwa kutumia taaluma hiyo alianza kujifunza kufanya upasuaji wa maiti ili kujifunza na kuzifahamu sehemu zinazounda mwili, ikiwamo ngozi, mishipa ya damu, ya fahamu, misuli na ogani za mwilini.Kutokana na mafanikio yake na umuhimu wake kuelekea katika fani ya tiba, somo la upasuaji wa maiti ulianza kutumika duniani katika vyuo vya tiba.Ingawa palitokea upinzani wa kidini wakitaka jambo hili lizuiliwe, paliwekwa taratibu maalumu zilizokubalika na kusimamiwa kisheria.
Upasuaji maiti
Wanafunzi wote wanaosoma sayansi ya tiba duniani mwaka wa kwanza hufanya upasuaji wa maiti ili kujifunza maumbile ya mwanadamu yalivyo, hii husaidia katika fani ya utabibu kwani maiti hizo zinakuwa ndiyo mgonjwa wa kwanza wa mwanachuo.
Mwaka 1831, ilihalalishwa kisheria kwamba miili iliyokosa ndugu au kutotambulika, itumike kwa wanafunzi wa chuo wanaosomea fani ya sayansi ya tiba.
Kwa bahati mbaya hapo baadaye ikaonekana maiti za namna hiyo si rahisi kuzipata huku mahitaji yakiongezeka.
Mwaka 1839 huko Chicago, Marekani ulianzishwa utaratibu maalumu wa kuomba watu kujitolea miili yao pale watakapofariki ili itumike kwa ajili ya kujifunzia maumbile ya mwanadamu. Zikawekwa kanuni na sheria kuhusu muundo mzima wa jambo hilo bila malipo. Taratibu hizo zilirithiwa sehemu mbalimbali duniani lakini hufanyika kwa usiri mkubwa.
Cadaver ni nini?
Ni maiti za watu ambazo hutumiwa na wanafunzi wa vyuo vya tiba kwa ajili ya wanafunzi kujifunza na kuona maumbile ya mwili mzima. (MWANANCHI)

No comments: