ANGALIA LIVE NEWS

Monday, July 14, 2014

GIGGS ATAKA NAMBA YAKE IENDELEE KUTUMIKA MANCHESTER UNITED

Mkongwe wa Machester United Ryan Giggs amesema asingependelea kuaona Club yake ya Manchester inatundika namba ya jezi yake kusudi isvaliwe na mchezaji mwingine

Giggs aliyeitumikia Man U kwa miaka 23 na aliyecheza mechi 963 amesema anatarajia kuona Manchester wanampatia mchezaji mwingine atakayetumia jezi namba yake na yeye binafsi angefurahia kuona ni mchezaji gani atakayetumia jezi namba yake na jinsi gani atakavyowakilisha Manchester United akiwa kwenye jezi namba yake aliyokuwa akiitumia wakati akiitumikia timu hiyo.

Wachezaji kama Bobby More, Paulo Maldin na Javier Zanetti ni wachezaji ambao club zao walizokuwa wakichezea haziruhusu mchezaji mwingine kutumia namba za jezi walizokuwa wakizivaa.

Giggs yeye amaesema angependelea kuona namba ya jezi yake inaendelea kuvaliwa na mchezaji mwingine atakayechezea Manchester.

No comments: