ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, July 8, 2014

HII NDO SARAFU MPYA YA TSH. 500/= ITAKAYOANZA KUTUMIKA HIVI KARIBUNI

Sarafu mpya ya Tsh. 500/=
Baada ya kuonekana noti ya shilingi 500 ina na mzunguko mkubwa wa matumizi na inachakaa kwa haraka huku kiwango chake cha kuhimili mizunguko ni miezi sita, Benki kuu ya Tanzania (BOT) inatarajia kubadili noti hiyo na kuifanya sarafu.
Sarafu hiyo ya 500 inatarajiwa kutambulishwa na kuanza kutumika July 2014 ikienda sambamba na kipindi cha mwaka huu wa fedha ambapo unaambiwa hii sarafu ikishatoka inatarajiwa kudumu kwenye mzunguko kwa zaidi ya miaka 20 na kubaki na ubora wake uleule, yani ni imara kuliko noti.
Noti ya 500 inayotumika sasa

Afisa mkuu wa benki kitengo cha idara kurugenzi za kibenki Patrick Fata ameongea na millardayo.com na kusema “Tunafanya hivi kwasababu noti ya 500 inachakaa haraka kulinganisha na mzunguko wake na kuwafikia watu wengi pia huchakaa haraka kutokana na mzunguko wa kushikwa na watu wanaofikia mpaka milioni moja kwa siku, hiyo ni idadi kubwa kuliko ya wanaoshika noti ya elfu 10 kwa siku’

3 comments:

Anonymous said...

Pesa ya Tanzania inazidi kua Pumba Kila Siku.. Before you know it,coins za buku 1, Buku 2 and kadhalika..

Uchumi tunao lakini serikali inaukalia, misaada kibao kwenye bageti tuna devalue hela yetu kila siku, unemployment ya kumwaga, vijana wenye nguvu hawana kazi, elimu nayo finyu,Import nyingi, Export chache, watu tunaowategemea kusimamia Nchi ni wafanya biashara, wanauza nchi yetu na kila kitu chake. siasa za kioga, kujipendekeza na chama kimoja kilichong'ang'ania mambo ya kizamani kinaendelea kutawala milele, wakichalenjiwa na watu wengine wanatoa vitisho, hakuna improvement, 1 step forward two steps back, Wakiambiwa Ukweli na hata viongozi wa nchi nyeningine inakua balaa(eg KAGAME & KENYATA), haoni ukweli kama hawa watu wanataka tuendelea kwa pamoja ila TZ haiko tayari na maendeleo, watu waendelea kuchekechua, tukitengwa kwenye Major project tunaanza kualalamika.

Kazi ya viongozi wetu ni kujipendekeza kwenye nchi kubwa as if we getting something important from them( they dont just give us for free) na kusafiri kila siku kwenda safari zisizo na umuhimua( what is the point kua na mabalozi na wawakilishi wa serikali kama 1 person has to travel to close all the deals as well as peach to the investors)

We cant stop now straight to the Bottom Now...MUNGU IBARIKI TANZANIA

Anonymous said...

Mdau wa kwanza.umeiangalia nchi kwa mapana na.marefu na kiukweli. Kama ujuavyo hakuna litakalo tendeka kwa maana nchi inatawaliwa ki mabavu, na walioamka na kulalamika huchukuliwa hatua mbalimbali. Walio wengi waoga ......ujasiri haupo kabisa. Inadvertently sikitisha sana. Tusalini haya mambo yaishe. Nchi jirani zote zimeamka na zinajaribu kutuamsha lakini wapii.....kazi ipo.

Anonymous said...

Twende mbele turudi nyuma, kuexport ni jukumu letu sio jukumu la serikali. Sisi ndio hatutaki kuwekeza tunang'ang'ania kuajiriwa na waarabu na wazungu wanaoexport. Kazi yetu kulalamika tu.