ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, July 1, 2014

JE SIKU UKIAMKA NA UKAKUTA KARIAKOO IMEKUWA CHINATOWN USISHANGAE NDIKO TUNAKOELEKEA

Pitapita ya Vijimambo New York na kutembelea mji unaoitwa Chinatown uliopo Manhattan, NYC na kujionea kila kitu kimeandikwa kichina ndipo Vijimambo ikakumbuka Watanzania wanavyolalama kuhusu Wachina na kuwatolea mfano wa kwamba wanakaba mpaka penati. Marekani ni Dunia ya kwanza lakini wao wameona umuhimu wa Wachina na kuwaruhusu kutengeneza miji yao karibu majimbo yote nchini Marekani na kila maandishi yameandikwa kwa lugha mbili, Kichina na Kiingereza na kila biashara ambayo Tanzania wanaita penati kwa maana ya kwamba hata zile kazi ambazo wanafikiria ni za wazawa Wachina wanafanya kwa Vijimambo haina tatizo na Wachina kufanya biashara hizo ili mradi zinatambulika kisheria na wanazilipia kodi.
 Hapa ni kama mtaa wa Congo, Kariakoo Wachina wameupamba mji wa Chinatown kwa vitu mbalimbali miji hii ipo karibu kila Jimbo la nchi hii.
 Hili ni duka la dawa upande mmoja limeandikwa Kichina na upande mwingine limeandikwa Kiingereza.
 Mpaka McDonald imeandikwa Kichina
 Mchina akiwa nje ya Duka lake mtaa wa Canal New York, NY
 Chinga wa Kichina akipiga box Chinatown.

 Kila kona ni Kichina kwa kwenda mbele.
 Ndio hivyo tena Kichina kimetawala kila upande wa mji.

No comments: