ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, July 1, 2014

BANDA LA JESHI LA MAGEREZA LANG'ARA KWA SAMANI ZA NDANI MAONESHO 38 YA BIASHARA YA KIMATAIFA JIJINI, DAR ES SALAAM

 Sofa seti iliyotengenezwa kwa Ustadi mkubwa na Mafundi Stadi wa Jeshi la Magereza kama inavyoonekana katika picha. Sofa hiyo imetengenezwa kwa kutumia Mbao aina ya Mkongo ambao ni imara na hudumu kwa muda mrefu zaidi.
 Kabati la Vyombo ambalo limetengenezwa kwa Ustadi mkubwa na Wataalam wa Jeshi la Magereza. Kabati hilo la Vyombo limetengenezwa kwa ubao aina ya Mninga.
 Meza ya chakula yenye viti sita iliyotengenezwa kwa kutumia mbao aina ya Jakaranda inayopatikana katika Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Mbeya na Iringa. Meza hiyo ya duara imetengenezwa na Mafundi Stadi wa Jeshi la Magereza katika Kiwanda cha Samani cha Arusha ambacho kinamilikiwa na Jeshi la Magereza.
 Kitanda kilichotengenezwa kwa Ustadi mkubwa na Mafundi wa Jeshi la Magereza. Kitanda hicho kimetengenezwa kwa mbao aina ya Jakaranda inayopatikana katika Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Mbeya na Iringa.

 Kiti cha kunesa Maalum kwa ajili ya Watu Wazima kinapatikana katika Banda la Jeshi la Magereza lililopo katika Viwanja vya Maonesho 38 ya Biashara ya Kimataifa, Jijini Dar es Salaam.
 "Dressing Table" iliyotengenezwa kwa Ustadi Mkubwa na Mafundi wa Jeshi la Magereza. Dressing Table hiyo imetengenezwa kwa kutumia mbao aina ya Jakaranda kama inavyoonekana katika picha(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
Banda la Jeshi la Magereza lililopo katika Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa, Jijini Dar es Salaam. Jeshi la Magereza linashiriki katika Maonesho ya 38 ya Biashara Mwaka 2014 ambapo Wananchi  wanakaribishwa kuja kutembelea Banda la Jeshi la Magereza ili waweze kupata bidhaa mbalimbali za Samani za ndani zenye ubora wa hali ya juu pamoja na bidhaa nyinginezo za ngozi zinazozalishwa na Jeshi la Magereza.

3 comments:

Anonymous said...

Jamani tuyapongeze magereza, geee huo ni ufundi wa hali ya juu kabisa. Do they do a follow up on where those people go after life in jail. Would be nice to know.

Anonymous said...

The only problem with these furnitures is their fixed nature, kwamba huwezi kuzifungua kama zile za IKEA. Mlango wa chumba ukiwa mdogo ndio hivyo tena Kochi aliingii. Ukiwa unasafiri umepata uhamisho ndio kasheshe. Wajitahidi kuweka flexibility kidogo.

Unknown said...

Naipata wapi dressing table hiyo? Nahitaji