Advertisements

Wednesday, July 30, 2014

LADY JAYDEE KAPATA TUZO SAWA NA ALIYO PATA DIAMOND ATAPOKELEWA KWA MIDUNDIKO NA MATALUMBETA?

Wasanii wa Tanzania wenye mashabiki wengi Afrika Mashariki, Lady Jay Dee na Diamond Platinumz, wameitoa Tanzania Kimasomaso kwa kushinda tuzo moja moja katika tuzo za AFRIMA (African Muzik Magazine Awards 2014), zilizofanyika jana Dallas, Marekani.

Kwa mujibu wa mtandao wa African Music Magazine, Lady Jay Dee alishinda tuzo ya mwimbaji bora wa kike wa Afrika Mashariki na Diamond Platinumz alishinda tuzo ya Msanii bora wa kiume wa Afrika Mashariki. JayDee atapokelewa kwa matalumbeta maana nae kiwatoa kimasomaso Watanzania hasa wanawake nao wajitume kwani inawezekana.
Lady Jay Dee alishinda tuzo ya mwimbaji bora wa kike wa Afrika Mashariki sawa na Diamond Msanii bora wa kiume wa Afrika Mashariki. 

1 comment:

Anonymous said...

unajua jay dee ana maringo sana na anadharau watu,ukiona wanamuziki wengi kwenye umati wa watu wanaenda wanasalimia watu wanasmile.but yeye anataka watu wamfate wambembeleze,lakini diamond hes very charming.na anawazoea watu vizuri,