ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, July 31, 2014

MAJAMBAZI 10 WANAOUNDA MTANDAO HATARI WA UHALIFU NCHINI WAMETIWA MBARONI, SILAHA MBALIMBALI ZAKAMATWA

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova akiongea na Waandishi wa Habari Huku akionyesha baada ya Silaha Kituo cha Polisi cha Kati Dar es salaam.


MAJAMBAZI 10 wanaounda mtandao hatari wa uhalifu nchini, wametiwa mbaroni wakati wa msako mkali uliofanikisha pia kukamatwa kwa silaha mbalimbali.

Silaha hizo ni bunduki tisa zikiwemo SMG tatu, bastola mbili, short gun nne na risasi 15 zilikamatwa.

Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, aliyasema hayo ofisini kwake kwenye mkutano na waandishi wa habari.

Majambazi hao wamekamatwa katika msako mkali unaoendelea jijini Dar es Salaam katika harakati za kuhakikisha kwamba maisha na mali za wakazi wa Dar es Salaam vinalindwa kikamilifu.

Katika msako huo watuhumiwa walisachiwa katika miili, makazi, na maficho yao na wakakamatwa na jumla ya silaha 9 kama ifuatavyo:-
SMG NO. 13975 ikiwa na risasi 11 na magazine 2
SMG 1 haikuwa na magazine na namba hazisomeki.
BASTOLA 1 aina ya LUGER yenye namba 5533K
BASTOLA 1 aina ya BROWNING yenye namba TZACR83494 S/No.7670 Na risasi 6 ndani ya magazine.
S/GUN PUMP ACTION na risasi 55
MARCK IV iliyokatwa mtutu na kitako yenye magazine 1 na risasi 4
BASTOLA 1 yenye namba A963858 browning ambayo ina risasi 1
SMG 1 ambayo iko kwa mtaalam wa uchunguzi wa silaha (Balistic)
SHOT GUN TZ CAR 86192 ilitelekezwa baada ya msako

Majina ya watuhumiwa ni ifuatavyo:-
1. MAULIDI S/O SEIF MBWATE miaka 23, mfanyabishara, mkazi wa Mbagala Charambe.
2. FOIBE D/O YOHANES VICENT miaka 30, hana kazi, mkazi wa Mbagara Kibondemaji.
3. VICENT S/O OGOLA KADOGOO miaka 30, mkazi wa Mbagara Kibondemaji
4. SAID S/O FADHIL MLISI – miaka 29, dereva wa Bodaboda, Mkazi wa Gongolamboto
5. HEMEDI S/O AWADHI ZAGA miaka 22, dereva wa Bodaboda, mkazi wa Gongolamboto
6. MOHAMED S/O IBRAHIM SAID miaka 31, Fundi welder mkazi wa Kigogo.
7. LUCY MWAFONGO. Miaka 41, mama lishe mkazi wa Vingunguti Ukonga
8. RAJABU S/O BAHATI RAMADHANI, miaka 22, Mkazi wa Kariakoo
9. DEUS JOSIA CHILALA miaka 30, Mgonga Kokoto Kunduchi , mkazi wa Yombo Kilakala.
10. MARIETHA D/O MUSA miaka 18, mkazi wa Yombo Kilakala
Mwanamke pekee katika kundi hilo anayejulikana kwa jina la FOIBE D/O YOHANES VICENT ameshiriki katika matukio ya uporaji wa kutumia silaha, mauaji, n.k. na yeye mwenyewe alikuwa akitumia bunduki aina ya SMG.
Katika baadhi ya matukio wananchi walioshuhudia matukio haya wamekuwa wakitoa taarifa kwamba alikuwepo mwanamke aliyekuwa akifyatua risasi na hatimaye polisi walifanikiwa kumkamata akiwa na wenzake katika kundi hilo.
Licha ya kukamatwa kwa mtandao huu hatari Jeshi la Polisi linaendelea na misako ya mitandao mingine ya ujambazi kwa madhumuni yaliyotajwa hapo juu.
Hivyo tunawashukuru wananchi kwa namna walivyoendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutokomeza uhalifu.
Majambazi hao watafikishwa mahakamani baada ya Mwanasheria wa Serikali kutafuta majalada yao ya kesi mbali mbali.
S.H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM

No comments: