Advertisements

Thursday, July 17, 2014

MASIKINI HAPPINESS MILLEN MAGESE!!!


JINA lake kamili anajulikana kama Happiness Millen Magese. Ni mshindi wa Shindano la Miss Tanzania Mwaka 2001.Happiness Magese (35), alikuwa akifanya kazi zake za uanamitindo nchini Afrika Kusini chini ya Kampuni ya Ice Model Management na alikaa huko kwa miaka nane kabla hajahamia katika Jiji la New York, nchini Marekani ambapo amesaini mkataba na Kampuni ya Ford Models mpaka sasa hivi. Ana miaka minne na tayari ameshaongezewa miaka miwili zaidi ya fani hiyo ya uanamitindo duniani.

Happiness Magese anasihi wanawake kucheki afya zao mara kwa mara wasije wakakutwa na tatizo kama lake la ugumba ambalo limeharibu na kibofu chake na kupelekea hata kushindwa kukojoa kwa njia ya kawaida na badala yake anatumia mipira, ni vema kuchek afya mara kwa mara

6 comments:

Anonymous said...

Pole sana dada, naoombeni mnielewesha jamani ugumba ni nini, (kuuliza si ujinga) Asanteni sana

Anonymous said...

Ushauri mzuri, na tunampa pole sana na apone kwa haraka. .

Anonymous said...

POLE SANA DADA H.MAGESSE. JIBU LA TATIZO LAKO NI YESU TU. NIKUPE MFANO WA JAMBO HILI ELEKEZI:- GARI YAKO IKISHINDIKANA KUTENGENEZEKA KWA DEALER HUIPELEKA WAPI? HUTAFUTWA MANUFACTURER.HUYO NDIYE HUJUA YOTE YA HILO GARI. HATA WEWE MAADAKTARI WAMESHINDWA KAMA BINADAMU LAKINI MUNGU HAJASHINDWA...
READ BIBLE, MARK 5:25-34.
PIA KWA USHAURI ZAIDI NIANDIKIE AU TUWASILIANE KWA EMAIL kipen_84@yahoo.co.
OK, na kuhusu mgumba au ugumba ni nini? Ni mwanamke yeyote mwenye uwezo wa kuzaa lakini akawa na complications za uzazi zinazotokana na aidha utoaji wa mimba za ujanani,magonjwa ya zinaa yaliyocheleweshwa kutibiwa,mke kuwa na acid nyingi ukeni na hata mji wa uzazi, mwingiliano wa homoni za kike na kiume ktk tezi moja ya uzazi. Tezi ya uzazi ya kike inatakiwa izalishe homoni za kike pekee yake na siyo mchanganyiko. Mwisho ugumba usikukatishe tamaa, utsa ndiyo ukatishe tamaa kama hauna Yesu.
ASANTENI SANA.....Ni mimi mtaalamu

Anonymous said...

With God nothing is impossible, My advise to you Happiness is that get a plane ticket to Nigeria and go and see The Prophet of Most High God TB Joshua and all shall be Well.

Anonymous said...

Ana ugonjwa wa kike unaoitwa Endometriosis. Sijui kwa Kiswahili unaitwaje. Kama haukutibiwa mapema unaweza sababisha Endomertail Cancer.

Kama unahitaji maelezo zaidi uliza tu bila wasi wasi na nitafurahi kukuelewesha

Anonymous said...

Wewe mtaalamu una scientific proof kwamba mimba za ujanani zikitolewa zinasababisha Endometriosis? ulifanya study wapi na reports ziko wapi? Acheni kujisingizia hapa eti mtaalamu, I read about this decease and the cause is not known. all the causes provided are guess work. Usihukumu wenzio, andika majina yako na CV yako tuone wewe ni mtaalamu wa nini. Pole Happyness, Mungu akuangazie, upate nafuu. Wengi wamesumbuka kwa matatizo mbalimbali ila watoto mtoaji ni Mwenyezi. Usikate tamaa.