Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchmbi (wa nne kutoka kushoto) akiwaongoza wadau
waliofika kuadhimisha sherehe za kuanza kwa ujenzi wa mradi wa barabara
ya kutoka Mayamaya Dodoma hadi Bonga Babati kwa kiwango cha lami kuomba
Dua ili mradi huo ukamilike kwa wakati bila kukwamishwa na changamoto
mbalimbali. Sherehe hizo zilifanyika mapema Julai Mosi, 2014
kijijini Kolo Wilayani Kondoa.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (wa pili kushoto) na ujumbe
alioambatana nao wakikagua magari yanayotumika kwenye ujenzi wa barabara
ya kutoka Mayamaya Dodoma hadi Bonga Babati kwa kiwango cha lami Mapema
jana wakati wa maadhimisho ya kusherehekea kuanza kwa ujenzi wa mradi
huo yaliyofanyika Kijiji cha Kolo Wilayani Kondoa, wengine pichani ni
wakandarasi wa Kampuni ya China Railway Seventh Group inayojenga
barabara hiyo kipande cha Bonga-Mela (88.8KM).
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akimkabidhi Dereva Abuu Ally
Funguo ya kuwashia mitambo ya kujengea barabara kuashiria kuanza rasmi
kwa Ujenzi wa Barabara ya kutoka Mayamaya Dodoma hadi Bonga Babati kwa
kiwango cha lami wakati wa kuadhimisha sherehe za kuanza kwa ujenzi wa
mradi huo zilizofanyika mapema Julai Mosi, 2014 kijijini Kolo
Wilayani Kondoa, Kulia anayeshuhudia ni Mbunge wa Kondoa Kaskazini Mhe.
Zabein Mhita.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (Katikati mwenye kilemba) na
ujumbe alioambatana nao wakipatiwa maelezo ya mradi wa barabara kutoka
Mayamaya Dodoma hadi Bonga Babati kutoka kwa wakandarasi wa Kampuni
inayojenga barabara hiyo ya China Railway Seventh Group wakati
alipotembelea kambi ya kampuni hiyo iliyopo kijiji cha Kolo Wilayani
Kondoa mapema Julai Mosi, 2014
Wakandarasi wa Kampuni ya China Railway Seventh Group inayojenga
barabara ya kutoka Mayamaya Dodoma hadi Bonga Babati kipande cha
Bonga-Mela (88.8KM) kwa kiwango cha lami wakisikiliza salamu ya Mkuu wa
Mkoa Dodoma (Hayupo pichani) wakati wa kuadhimisha sherehe za kuanza kwa
ujenzi wa mradi huo zilizofanyika Julai Mosi, 2014 kwenye Kijiji
cha Kolo Wilayani Kondoa.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, wadau, Mafundi na Wataalamu wa Kampuni ya China
Railway Seventh Group inayojenga barabara ya kutoka Mayamaya Dodoma hadi
Bonga Babati kwa kiwango cha lami kipande cha Bonga-Mela (88.8KM)
wakiwa kwenye picha ya pamoja muda mfupi baada ya kumalizika kwa sherehe
za kuanza kwa ujenzi wa mradi huo wa barabara zilizofanyika Kijijini
Kolo Wilayani Kondoa Mapema Julai Mosi, 2014.
Sehemu ya Wananchi wa Kijiji cha Kolo Wilayani Kondoa waliojitokeza kwa
wingi kuadhimisha sherehe za kuanza kwa ujenzi wa mradi wa barabara ya
kutoka Mayamaya Dodoma hadi Bonga Babati kwa kiwango cha lami
wakisikiliza salamu za Mkuu wa Mkoa Dodoma (Hayupo pichani), Sherehe
hizo zilifanyika mapema Julai Mosi, 2014. Picha na John Banda wa Pamoja Blog
No comments:
Post a Comment