Advertisements

Saturday, July 26, 2014

NIPO TAYARI KUWA NA URAFIKI NA MTU YEYOTE ATAKAYEKUA TAYARI KUWA KARIBU NA MIMI ROSE NDAUKA AFUNGUKA

Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Rose Ndauka.MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Rose Ndauka ameweka wazi kwamba kinachomfanya aishi vizuri na wenzake ni kutoendekeza makundi. Akipiga stori na mwandishi wa gazeti hili, Rose alisema 
anampenda na atampenda mtu yeyote atakayekuwa tayari kuwa na urafiki naye kwa sababu hiyo ndiyo staili yake ambayo inamfanya hata wanaomchukia katika makundi hayo wampende.“Nampenda kila mtu na nipo tayari kuwa na urafiki na mtu yeyote atakayekuwa tayari kuwa karibu na mimi, makundi hayana maana kabisa zaidi ya majungu tu,” alisema Rose.

No comments: