Advertisements

Thursday, July 31, 2014

PONGEZI KWA MHESHIMIWA RAIS KWA KUTUNUKIWA TUZO YA MWANA DEMOKRASIA BORA AFRIKA



Mhe. Dr Jakaya Mrisho Kikwete


Chama Cha Mapinduzi Tawi la Texas tunatoa pongezi zetu za dhati kwa 
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Dr Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutunukiwa tuzo ya mwana demokrasia bora Afrika.

Tuzo hii ni ishara ya kutambuliwa na kuthaminiwa kwa mchango wa Mhe. Rais na Watanzania wote kwa ujumla katika juhudi za kudumisha na kuendeleza demokrasia barani Afrika, hii ni heshima ya kipekee kwa Rais wetu na Watanzania wote.



Tunakuombea kwa Mwenyezi Mungu azidi  kukupa afya njema, hekima na busara zaidi kuitumikia nchi yetu na Afrika kwa ujumla.



Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki Afrika



KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI


Imetolewa na: Abdallah Nyangasa, Katibu
Tawi la CCM Texas.

No comments: