ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, July 20, 2014

TAIFA STARS NA MSUMBIJI NGUVU SAWA

Timu ya Taifa ya Tanzania leo imetoka sare baada ya kufungana bao 2-2 na timu ya Taifa ya Msumbiji katika mechi iliyokuwa na ushindani mkali mwanzo hadi mwisho katika kuwania nafasi ya kucheza katika kombe la Mataifa Africa 2015. Mabao ya Tanzania yamefungwa na mchezaji machachari Khamis Mcha yote katika dakika ya 65 na 71 kwa mkwaju wa penati huku magoli ya Msumbiji yakiwekwa kimiani na Elias Pelembe dakika ya 47 kwa mkwaju wa penati na Isack Carvalho dakika ya 87.

 Mchezo ulikuwa mkali na timu zote zilishambuliana kwa zamu huku na mpaka kufikia mapunziko timu zote zilikua hazijafungana. Kipindi cha pili kilianza kwa Msumbiji kupata bao la kuongoza kwa mkwaju wa penati na baadae timu ya Tanzania ilisawazisha bao hilo na kuongeza bao lingine lililopatikana kwa mkwaju wa penati na baadae Msumbiji ikasawazisha zikiwa zimebakia dakika 3 mpira kuisha.

No comments: