ITAKUWA balaa! Siku chache kuelekea kwenye Tamasha la Matumaini, Agosti 8, mwaka huu, mastaa kibao watakaolipamba jukwaa litakalofungwa ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar, wameeleza jinsi gani
Yemi Alade
Diva wa muziki kutoka pande za Nigeria ambaye huwa habahatishi, amesema: “Nitawapagawisha mashabiki kwa kupiga nyimbo zangu zote kali ikiwemo iliyojizolea umaarufu kila kona ya Afrika, Johhny. Mashabiki wategemee kumuona Yemi akimaliza. Kati ya nyimbo ambazo nitazipiga ni Tangerine, Johnny, Bamboo, Birthday, Ghen Ghen Love na nyingine kibao.”
Ali Kiba
“Kwa mara ya kwanza, nitapanda jukwaa la Uwanja wa Taifa kuweka historia mpya. Mashabiki wengi ‘wamenimiss’, Agosti 8 itakuwa maalum kwa ajili yao. Wategemee ngoma kali kibao kutoka kwa mfalme wa Bongo Fleva niliyerudi kupangusa kiti changu na kukikalia,
“Nitagonga kali kama Dushelele, Single Boy, Run Dunia na mpya zinazobamba kwa sasa ambazo ni Mwana na Kimasomaso.”
Shilole
“Mashabiki wategemee kuona shoo ya nguvu, hakuna anayebisha kwamba najua kuimba na kukitumia vyema kiuno changu. Nitazipiga Chuna Buzi, Paka la Baa, Nakomaa na Jiji, Lawama na hii mpya ya Namchukuwa.”watakavyolishambulia jukwaa.
R.O.M.A“Huwa sibahatishi katika shoo zangu, nitawainua mashabiki kwa kunyoosha kidole cha mwisho juu kwa kupiga ngoma kali kibao kama Tanzania, Mechi za Ugenini, Pastor, Mr. President pamoja na hii mpya ya Karibu Kwenye Karamu (KKK).
Navy Kenzo
“Tutawapagawisha mashabiki kwa staili ya Bokodo iliyotokea kujizolea umaarufu mkubwa. Ngoma kama Cheza Kizembe, Usinibwage, Chelewa (Bokodo) na hii mpya ya Aiyola ndizo zitakazosisimua zaidi siku hiyo.”
Juma Nature
“Huwa ushindi kwetu ni lazima, tutakamua Tatu Bila, Fitina, Nyama pamoja na ngoma mpya niliyomshirikisha Lady Jay Dee, Kama Jana.”
Scorpion Girls
“Sisi huwa hatubahatishi, unapomuona sehemu Isabela na Jini Kabula ujue timu nzima ya Scorpion Girls imetimia. Tutacheza na kuwaimbia nyimbo zetu kama Tanzania, Watuache na nyingine kibao.”
Madee
“Pale taifa nitakwenda kudhihirisha urais wangu wa Manzese, nitazipiga zote kali ikiwemo Pombe Yangu, Tema Mate Tuwachape na hii mpya ya Ni Shidaa, noma saaana!”
Meninah
“Nitawapagawisha kwa ngoma zangu kali kama Dream Tonight, Kacopy Kapaste na mpya ya sasa ambayo ni Pipi ya Kijiti. Tukutane pale taifa, Agosti 8 mwaka huu.”
No comments:
Post a Comment