ANGALIA LIVE NEWS

Friday, July 4, 2014

TANGAZO LA DINA MARIOS "DADA DINA"


Habari za leo,natumaini upo salama.Napenda kuchukua nafasi hii kukushirikisha sehemu ya shughuli zangu za kijamii.Mwaka jana nilianzisha kitu kinachoitwa dada dina cares.Hii ni baada ya kushinda tuzo ya mwanamke wa mwaka na nikapewa zawadi ofisini kwangu tsh ml 2 ili niifanyie chochote ntakacho taka.Ila mie niliamua kuitumia kwa ajili ya kununulia mahitaji mbali mbali muhimu watoto yatima wanaolelewa katika vituo kadhaa.Pia nilishirikisha wadau mbali mbali kufanikisha hilo.Nilichangisha pesa kwa muda wa wiki tatu ambayo niliweza kuhudumia vituo vitatu vya watoto yatima nilivyowanunulia mchele kg 100,unga kg 100,maharage kg 100,sukari kg 100,mafuta ya kupikia litre 40,dawa za meno,mafuta ya kujipaka,sabuni za kufulia box 10,mashuka,magodoro,vitanda,neti,nyavu za madirisha,nguo bila kisahau vifaa vya shule.Vyote hivi kila kituo kilipata kwa idadi hiyo.
Sasa basi nakukaribisha tena katika mchakato huu ambao tutahudumia vituo vitano vya watoto yatima.Lengo ni kuhakikisha hawa watoto wanapata mahitaji yao ya msingi.Walezi wanaolea hivi vituo hawana uwezo wa kuwapa mahitaji yote muhimu hawa watoto ila mimi na wewe kwa sababu hatuwezi kuwachukia kuishi nao basi tunawezesha kuwapa wepesi hawa walezi kuendelea kuwalea.Kama upo tayari kuchangia tafadhali nijibu ili nutachangia.Kwa kiasi chochote utakachobarikiwa.
Tukimaliza kupeleka mahitaji yao watoto hawa watakutana katika toto party matata sana itakayoambatana na chakula cha mchana na michezo mbali mbali na wewe ukiwa sehemu ya wahudhuriaji wewe na familia yako pia ikiwezekana.
NAMBA ZA KUCHANGIA NI 0759789863 na 0657795654 Zitaonyesha jina la Halima Temu.Ni namba tumesajili kwa jina la huyo dada maana toka mwaka jana amekuwa akinisaidia hili zoezi la kukuaanya michango.
Pia unaweza kutuletea nguo za watoto zilizo katika hali nzuri sio zilizochanika au kipauka sanaa.
Natanguliza shukrani zangu za dhati endelea kutembelea hapa ili kujua ni vituo gani yunavyovichangia zoezi litadumu kwa muda wa wiki tatu tu.

No comments: