Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mark Simmonds, alitoa ahadi hiyo jana wakati akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada ya kutembelea mbuga ya wanyama ya Selous.
Alisema Uingereza itakuwa inatoa ruzuku ya kukabiliana na vitendo vya ujangili baada ya kufanyika kwa tathimini kuona kiasi gani cha fedha kinahitajika ili kizazi kijacho kisije kuangalia tembo kwenye picha.
Simmonds alisema baada ya kutembelea mbuga ya Selous amebaini kuwa askari wanaoimarisha ulinzi katika mbuga hiyo wanapata kero nyingi na kwamba hivi karibuni kutafanyika mkutano wa kujadili namna ya kukabiliana na vitendo vya ujangili utakaofanyika Botswana.
Uingereza imekuwa moja ya nchi zilizowekeza kwa kiwango kikubwa Tanzania ambapo asilimia 37 ya fedha zake zinaingia moja kwa moja Tanzania.
Alisema Uingereza imechangia nchi tano katika kuimarisha uhusiano wa kimaendeleo na Tanzania ikiwa mojawapo na maeneo muhimu yaliyochaguliwa kusaidia ni kilimo, gesi, mafuta na biashara.
“Uingereza inasaidia pia katika Mpango wa Rais wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN),imesaidia kupatikana kwa ajira 275 na walimu wapya 35,000, Paundi milioni 130 zimewekezwa katika kilimo,”alisema.
Kwa uapnde wake Waziri wa Maliasili ya Utalii, Lazaro Nyalandu, alisema serikali imejipanga kukabiliana na vitendo vya ujangili na inapata mafanikio makubwa kwasababu inashirikiana na mataifa mengine katika vita hiyo.
Alisema hivi sasa serikali imetoa bunduki aina ya AK47 zipatazo 500 zinazotumika kulinda hifadhi za taifa na kwamba silaha na vitendea kazi zaidi vitaongezwa kulingana na jinsi majangili wanavyojipanga kuendeleza vitendo hivyo.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
1 comment:
watasaidia na wao watachota humu humo hizo ndovu na kuzisafirisha kwao
Post a Comment