Advertisements

Saturday, August 30, 2014

FLORA AFUNGUKA NA KUSEMA MIMBA ALIYO NAYO NI YA MBASHA NA SIYO YA GWAJIMA

Muimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Flora Mbasha 
Muimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania ambae pia ni Mke wa Emmanuel Mbasha amefunguka na kusema kuwa hana mahusiano yoyote ya kimapenzi na na Mchungaji wa Kanisa la kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima,Flora amesema hayo alipokuwa akichat Live kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV katika kipengele cha Kikaangoni Live .
Flora amesema kuwa hawezi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu ambae ni ndugu yake hivyo Mchungaji Gwajima ni mjomba wake na si mpenzi wake kama ambavyo watu wamekuwa wakizusha kwa lengo la kumchafua na kumshushia hadhi."Hayo ni maneno tu ya watu mtaani ila MchungajiGwajima ni mtumishi wa Mungu na ni uncle wangu ninawezaje kuwa na mahusiano na uncle wangu..? "Alihoji Flora.
wakati akijibu ya maswali ya mashabiki ambayo mengi yao yalikuwa yakimtuhumu na huku watu wengi wakitaka kujua ukweli juu ya ugomvi uliopo kati yake na Mumeo kama ni kweli au ni skendo tu za magazeti,Flora aliweka wazi kuwa kuna vyombo vya habari ambavyo vimekuwa na lengo la kumchafua na kumualibia sifa ndio maana walitumia gharama kubwa kufanya wanavyoweza ili kutimiza malengo yao,mbasha amedai kuwa alimua kukaa kimya kwa kuwa hakukuwa na ukweli wowote.

1 comment:

Anonymous said...

Anatakiwa kufanya DNA ili kupata ukweli kama mimba ni ya mme wake