Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita,Peter Kakamba
Mauaji ya watu yamezidi kutikisa katika vitongoji vya mji wa Geita, mkoani Geita hususani vijiji vilivyozunguka migodi ya dhahabu, baada ya juzi usiku mama na mkwewe mjamzito kuuawa kwa mapanga na watu wasiojulikana.
Mauaji hayo yametokea katika kata ya Nyarugusu wilayani Geita kitongoji cha Mwabasabi kwenye kijiji cha Ililika.
Watu hao wasiojulikana walienda katika kijiji hicho saa 2:30 usiku wakiwa na silaha za jadi, na kuanza kuwacharanga kwa mapanga kwa staili moja mwilini hadi kuwaua.
Waliioshuhudia tukio hilo walisema baada ya watu hao wakiwa kundi kubwa, walienda eneo la tukio na kuwakuta wakipata chakula cha usiku na kuanza kuwashambulia kwa kuwakatakata kwa mapanga hadi kuwafika na umauti kabla ya kutoweka kusikojulikana.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Peter Kakamba, alisema baada ya kupata taarifa hizo, jeshi lake limeanza uchunguzi wa kuwapata watuhumiwa wa tukio hilo.
Kakamba aliwataja waliouawa katika tukio hilo ni Nyanjige Mutula (70) pamoja na mkwewe Grace Hayo (18), aliyekuwa mjamzito. Hata hivyo, Kakamba alisema chanzo cha mauaji hayo bado hakijafahamika ingawa juhudi za jeshi lake kuwasaka waliohusika na kubaini chanzo cha mauaji zinaendelea.
Awali akizungumza katika eneo la tukio, Afisa Mtendaji wa kijiji cha Ililika, Fabian Mugeta, alisema tukio hilo ni la pili la mauaji ya kikatili kutokea kijijini hapo.
“Tunachoshangaa ni kuona wauaji wanatumia staili moja ya ukataji mapanga katika miili ya waliouawa,” alisema Mugeta.
Alisema mwishoni mwa Desemba mwaka jana, wanawake wawili ndugu, waliuawa kwa kukatwakatwa mapanga usiku katika kjijiji hicho. '”Hii ina maana wauaji hao ni wa aina moja kutokana na kutumia mtindo mmoja wa mauaji, huu ni mtandao mmoja unaotekeleza mauaji haya,'” alisema.
Marehemu hao walikatwa mapanga shingoni, mbavuni, kichwani, mabegani na vifuani, hali iliyoibua simanzi kubwa kwa wananchi.
Mume wa marehemu Grace, Kulwa Sanyenge, alisema wakati ukatili huo unatendeka hakuwepo nyumbani.
'”Inasikitisha mke wangu niliyemuoa mwaka jana, anafariki akiwa na ujauzito wa miezi mitano…lakini siyahusishi mauaji haya na imani za kishirikina ama kisasi,” alisema Sanyenge.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment