ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, August 26, 2014

MAMA SALMA KIKWETE AKUTANA NA MAMA GRACA MACHEL KWENYE OFISI ZA WAMA

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimpokea Mama Graca Machel aliyemtembelea kwenye ofisi za WAMA tarehe 25.8.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na mgeni wake Mama Graca Machel wanaonekana wakifurahia jambo kabla ya kupiga picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya WAMA.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mgeni wake Mama Graca Machel na wajumbe wawili wa Bodi ya WAMA. Wajumbe hao ni Mheshimiwa Sophia Simba,Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto (kulia) na Mama Hulda Kibacha (wa kwanza kushoto).
Mama Garaca Machel akiweka saini kitabu cha wageni wakati alipotembelea ofisi za WAMA tarehe 25.8.2014.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Bodi ya WAMA akimkabidhi zawadi ya picha mgeni wake Mama Graca Machel aliyemtembelea ofisini kwake tarehe 25.8.2014.
Mkurugenzi wa Idara ya Afya ya WAMA, Dkt. Sarah Maongezi (kulia) akitoa taarifa ya utendaji kazi wa idara hiyo kwa Mgeni Mama Graca Machel huku Mama Salma Kikwete na wafanyakazi wengine wakisikiliza.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Mgeni wake Mama Graca Machel kwenye ofisi za Taasisi hiyo zilizoko karibu na Ikulu.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi baadhi ya majarida yanayochapishwa na Taasisi ya WAMA kwa Mgeni wake Mama Graca Machel.
Mama Garaca Machel akimongeza mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete kwa kazi nzuri zinazofanywa na Taasisi yake.
Picha ya pamoja kati ya Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na wafanyakazi wa Taasissi ya WAMA na Mama Graca Machel na ujumbe wake mara baada ya kufanya mgeni uyo kutembelea ofisi hiyo tarehe 25.8.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimwaga Mgeni wake Mama Graca Machel wakati akiondoka kwenye ofisi ya WAMA baada ya viongozi hao kufanya mazungumzo.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuagana na Mgeni wake Mama Graca Machel nje ya ofisi za WAMA tarehe 25.8.2014.
PICHA NA JOHN LUKUWI.

No comments: