ANGALIA LIVE NEWS

Friday, August 15, 2014

Masanja naye apigilia msumari ndoa ya Diamond Platnumz na Wema Sepetu

Masanja naye apigilia msumari ndoa ya Diamond Platnumz na Wema Sepetu.
Baada ya uhusiano wa Diamond na Wema kuingia katika misukosuko na Diamond kutoa ujumbe mzito kumhusu wema sepetu, mchekeshaj maarufu hapa bongo Masanja mkandami ameamua kufua ya moyoni kuhusiana na uhusiano wa wawili hawa.
Masanja alisema haya “Street Pastor Anasema.. HILI SWALA LA DIAMOND NA WEMA NADHANI MUNGU AMEMUHURUMIA MMOJA WAPO KATI YA HAO WAWILI. KAMA WANGEKUWA WATU WA KUOANA WANGESHA OANA UCHUMBA GANI MREFU KAMA WANASOMEA UDOKTA???? RAFIKI YANGU NASIB, KAMA KWELI MLIPENDANA KWA DHATI HIZO KASORO ZINAREKEBISHIKA, MAANA HAKUNA MWANADAMU ALIYE SAHIHI KWAN HATA WW NASIB UNAMAPUNGUFU YAKO. NA WEWE DADA YANGU WEMA LAZIMA UJUE MME NDIO KICHWA CHA NYUMBA KWA MAELEZO HAYO INAONYESHA HAUMSIKILIZAGI MWENZIO OMBA MSAMAHA TENAAA NA TENA NA UKUBALI KUBADILIKA. MI SIPENDI MKIWA MNAONGOZANA WOTE KWENYE MA SHOW YA USIKU MME KAFANYE KAZI MKE ABAKI HOME UKIRUDI MWILI UMEPOA HATA UJAUZITO UNAINGIAA!! SASA WOOTE STEJINI MKIRUDI MIILI YA MOTO SI MTAZAA POPOMPOO JAMANIII!! NITAFURAHI KUSIKIA TOFAUTI ZENU MMEZIMALIZA KWA AMANI ILI MASHABIKI WENU WASIJISIKIE VIBAYA.”

1 comment:

Anonymous said...

umenena ukweli mtupu masanje na unaakili nzuri za kuona mbali big up my man.siyo kama yule mwenye akili za sisimizi mvuta bangi aliyemshauri nasib asione kisa atashuka kimuziki.mungu akitaka ushuke utashuka tu hata usipoowa mbona yeye hajaowa mbona yuko hivyo hivyo.

masanja kwa kweli wewe ndo unayetakiwa uwe rafiki na nasib ni mshauri wa kweli kabisa.

na kama kuowana wangeshaowana labda wanataka kuuza magazeti.

na nikweli mume ni kichwa cha familia lakin awe na busara si mume mchepuku asiye na hikma.

umenichekesha kweli kwa kusema watazaa popo mtu na si siri kila mtu stejini kila kukicha wazimu wazimu tu,ndo matatizo ya kuwafuata wazungu majuu kwa tabia zao mtu ukasahau mila za kwenu.

wema kwa kweli libukeni sana huyu na pia diamond wote wamekutana.

mambo ya ngoso mwachiiye mwenyewe ngoso watakuja kujuwana kama wanataka kuowana au vipi wache wachepuke mpaka wapate wanachokipata wanadhani ujana na uzima uko milele mmoja wao akiteguka kiuno au kupata kile tutaona kama kweli watapendana hawa.

hawana mpya.