ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, August 24, 2014

MASHABIKI WAMUUA MCHEZAJI ALGERIA

Timu ya Algeria ilipoishinda Urusi katika kombe la Dunia Brazil
Mchezaji mpira kutoka Cameroon amekufa baada ya kupigwa kichwani wakati mashabiki waliokereka waliporusha mawe mwisho wa mechi ya ligi ya Algeria.

Albert Ebosse, aliyekuwa na umri wa miaka 24, ndiye aliyetia magoli mengi kabisa katika ligi ya Algeria msimu uliopita.

Alirushiwa kitu wakati mashabiki walipokerwa kuwa timu yake, JS Kabylie, iliposhindwa kwa magoli mawili kwa moja katika mechi iliyochezwa nyumbani, Tizi Ouzou.

Yeye ndiye aliyepata hilo goli moja kwa timu yake.

Wizara ya mambo ya nchi ya Algeria imeamrisha uchunguzi ufanywe.

Ligi ya Algeria imefunga uwanja wa mpira wa timu ya JS Kabylie na imeitisha mkutano wa dharura Jumatatu.

No comments: