Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, leo amefanya mazungumzo na Bwa. Ahmad Al Julfar, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya simu ya Etisalat Jijini Dubai.
Katika mazungumzo yao, Mhe. Mjenga amemuomba Bwa. Julfar kuongeza nguvu ya uwekezaji na kupanua wigo wa huduma za kampuni ya simu ya Zantel ambayo Etisalat ni mwekezaji mbia, ili kupanua soko la wateja na kuboresha huduma.
Aidha, alimuomba kuangalia uwezekano wa kampuni ya Etisalat kuanza kuajiri wafanyakazi kutoka Tanzania na kuja kufanya kazi Dubai. Amemhakikishia Mhe. Mjenga kuwa atamuomba Mkurugenzi wa Etisalat anayeshughulikia rasilimali watu kufanya kikao na Ubalozi Mdogo ili kueleza nafasi zilizo wazi na kuanza kampeni ya kuajiri kutoka Tanzania.
Mhe. Mjenga amemshukuru kwa kubali ombi hilo, kwani, kitendo hicho si tu kitasaidia Watanzania kupata ajira bali kuimarisha uhusiano wa nchi zetu mbili.
No comments:
Post a Comment