Advertisements

Friday, August 29, 2014

Mwaliko Usiku wa Jakaya


2 comments:

Anonymous said...

Siyo nia na lengo langu kuzungumzia mantiki ya kuandaa sherehe ya kumpongeza Rais Kikwete kwa "kazi nzuri aliyowafanyia Watanzania huko nyumbani". Ningetegemea Watanzania wenyewe wenyeji na wakazi wa huko Muheza, Nyarugusu, Mahenge, Usagara, Ngara, Nanyumbu, Kiomboi, au Malagarasi pamoja sehemu nyingi kama hizo Tanzania Bara na Visiwani ndiyo waseme na kuafiki kwamba kweli wamenufaika na uongozi wake katika kipindi hiki cha miaka 10 iliyopita. Hilo ni suala jingine, lakini hoja yangu ya msingi ni kwamba sisi Wanadiaspora tuseme ukweli na kuambizana ukweli kuhusu Rais Kikwete na msimamo wake juu ya suala la Uraia pacha. Je, ni kweli kwamba anayo nia thabiti ya kutetea suala hili muhimu ambalo linagusa maisha yetu na ya ndugu zetu huko nyumbani? Je, ni kweli kwamba Rais Kikwete ameonyesha kwa dhati na kwa vitendo dhamira ya kupatikana kwa uraia pacha na kuboresha mazingira ya uwekezaji wa Wanadiaspora huko nyumbani ili aweze kustahili kupongezwa kwenye hoteli ya JW Marriot Washington DC hiyo tarehe 19 Septemba 2014!

Jibu unalo wewe mwenyewe.

Anonymous said...

Asanteni, Huyu mheshimiwa ameshindwa kazi ya kuwattetea WaTanzania sasa kuna haja gani ya kuja kukaa naye kupoteza muda yaani tunamsindikiza kumaliza muda wake na kutuachia machungu???