Mshambuliaji Emmanuel Okwi, raia wa Uganda ambaye juzi jioni alijiunga na Simba kudai kuwa atapambana na Wanajangwani hao kuhakikisha haki yake inapatikana.
Maneno hayo ya Okwi yamekuja baada ya kudai kuwa Yanga imevunja naye mkataba kisha kumfungulia mashtaka katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa madai ya kushindwa kuzingatia makubaliano yake na klabu hiyo kwa mujibu wa mkataba wake.
Okwi amesema atahakikisha anapambana Yanga hadi hatua ya mwisho kuhakikisha anapata haki yake.
Alisema klabu yoyote ile inapoingia mkataba na mchezaji inatakiwa kumlipa fedha zake zote za usajili kwa mujibu wa makubaliano na siyo kumzungusha na kufanya mambo yake kama viongozi wake wanavyotaka.
“Sina hofu kabisa juu ya jambo hili, naamini haki itapatikana kwa sababu hayo ambayo Yanga wananipakazia hayana ukweli wowote na kama kuna ukweli basi kutakuwa na sababu.
“Hata hivyo kwa sasa haina haja ya kuongea mambo mengi ila jambo la msingi ambalo ningependa kusema ni kwamba, nipo tayari kusimama sehemu yoyote ile juu ya jambo hili ili kuhakikisha haki yangu inapatika.
“Hata kama TFF na Fifa watanihitaji leo hii nitasimama mbele yao na kutoa ushahidi wangu juu ya jambo hili,” alisema Okwi ambaye Yanga imeachana naye akiwa bado na mkataba wa mwaka mmoja na nusu.
Yanga ilimsajili Okwi akitokea SC Villa ya Uganda ambayo alijiungana nayo akitokea Etoile du Sahel ya nchini Tunisia ambayo alikuwa na matatizo nayo.CREDIT:MWANASPOTI
No comments:
Post a Comment