ANGALIA LIVE NEWS

Monday, August 11, 2014

RIPOTI KAMILI YA KAMATI YA UCHAGUZI DMV


UCHAGUZI 2014
DMV
KAMATI YA UCHAGUZI


RIPOTI YA MATOKEO KWA BODI YA DMV
1:  Jana  usiku kwenye saa 5  hivi Kamati ilitangaza takwimu za awali za kura zilizopigwa ( za kituoni na za ghaibu) na wanachama hai wa jumuia. Ifuatayo ni matokeo kulingana na kila mgombea:
Jasmine Rubama (mweka hazina): 379- hakuwa na mpinzani
Ismail Mwilima (katibu): 171
Saidi Mwamemde ( Katibu): 251
Solomon Cris ( katibu): 167
Bernadeta Kaiza (makamu wa katibu): 254
Salma Moshi (makamu wa rais): 94
Harriett Shangirai (makamu wa rais): 333.
Katika nafasi za Katibu, Makamu wa Katibu na Makamu wa Rais, washindi wote walipata takriban kura  1 ½ kwa kila kura  1 ya mpinzani wake.
2: Kura za Rais:
Kura za rais zilionekana na utata ambao  ulizuia Kamati kutoa tangazo rasmi jana na ukalazimisha Kamati  kutekeleza  ukaguzi wa ndani wa mfumo wote wa kupiga kura ili kubainisha hitilafu katika urari wa takwimu za kura:
Yafuatayo ni matokeo ya ukaguzi  wa mfumo wa kura uliobainisha hitilafu:
a)  Idadi ya wapiga kura walioko kwenye orodha ya wanachama  hai:   586. Wanachama 150 waliamua kutopiga kura.
b) Wanachama waliopiga kura kituoni: 436
c)  Kura za ghaibu ( in absence): 14 Mgawo wake ni:  Libe 9 na Iddi 5
d) Kura zilizo toka kwenye masanduku na kuhesabiwa na mawakala: 445:  Katika hizo mawakala wa Libe waliripoti kura 214, na wa Iddi waliripoti kura 231:  Kwa hivyo kuna kura za ziada  kwenye masanduku kuliko idadi ya wapiga kura.  Ziada hiyo ni kura 9.
Kwa jumla:  Kura za Iddi ni 231 +5= 236
                Kura za Libe: 214 +9=223

6 comments:

Anonymous said...

Jamani apa lazima tuambiane ukweli na hii iwefundisho kwa watu watakao gombea any position in future ,hata siku moja usitegemee akilini kwako umuombe mtu akupigie kura na wewe ukamuamini yule mtu ukajua atakupigia umeshamuweka kwenye mahesabu yako na umesha jipa matumaini ,na hela umesha mtolea ya kujiandikisha kupiga kura je yule mtu unafikiri ndio atakuchagua ? wengine wanadanganya awataki kuweka uwadui wanadanya nitakupigia usiwe na wasi wasi lakini anapo piga kura unakua humuoni kwa hiyo hapo unakua tayari umeshatiwa mchanga wamacho matokeo yake hukubali matokeo kisa unasema nilikua nawatu wangu wengi waliniakikishia wata ni votia uliingia nao ndani ? uliwaona kama walikuchagua wewe au wali mchagua mpinzani wako ? ili ndio tatizo kubwa nimeliona apa DMV ni bora wale watu wanao kwambia sikupigii kuliko wale wanao kupaka mafuta ya mgongo ni hayo tuu ndugu zanguni kuwekeni makini sana na DMV akuchekae ndio adui yako japo atupendagi kuambiwa ukweli Dj Naomba usibanie comment yangu hili ni somo kwa wote tafadhali .

Anonymous said...

Ndiyo maana kama mliona team LIBE walikuwa wanafata watu ndani ya chumba cha kupigia kura. Na kuna watu wawili wamenipigia kuniambia kuwa LIBE kawalipia lakini HAWATAMPA KURA SABABU HAWAMJUI.... KAMA TUNGETAKA KUBLOW THE WHISTLE Huu uchaguzi wagombea wengine wangetolewa maana kumlipia mtu ni kutoa hongo.. mdau wa kwanza nakuunga mkono kabisa HILI LIWE FUNDISHO KWA WATU KUTAKA KURUBUNI UCHAGUZI... Na kaka Kessy wewe ndiyo wa kulaumiwa chumba cha kupigia kura ni yule mwenye karatasi tu ndiye anayetakiwa kuingia huko unless ana ulemavu wa macho na anahitaji msaada wa kusoma jina.....

ASANTENI WANA DMV KUTUCHAGULIA MAJEMBE IMARA!!!

Anonymous said...

Poleni wote mlioshindwa kwenye uchaguzi sio mwisho wa maisha na still mko part ya jumuiya ya DMV, inawauma sana kukosa ushindi kwakuwa mlinunua watu, mdau aliyetoa maoni kaongea vizuri, ukinilipia ada ya unachama sio guarantee nikuchague kwani sio jukumu lako wewe mgombea kunilipia mimi mpiga mkura,ni JIKUMU LANGU MPIGA KURA KULIPIA ADA YA UANACHAMA.JIFUNZE,KURA HAZINUNULIWI,

Anonymous said...

CASE ARRESTED! MDAU WA KWANZA UMENICHEKESHA!!

Anonymous said...

Mdau apo juu umeongea ukweli mtupu maana kuna mtu alikua anahesabu watu wa team fulani anatest na kuwajulisha wenzanke mpaka sasa hivi watu wetu walio piga kula ni 150 jamani jamani tunakua kama atujaenda shule hivi kweliwale watu unafikiri wote watakupigia wewe na wewe mwenyewe unajipa matumaini kabisa mpaka sasa hivi watu wangu 150 wameshanipigia wakati wengine wamempigi MTU MWINGINE jamani badilikeni state jingine wanatuona the super mburulaz wapo DMV kumbe ni wachache tuu .

Anonymous said...

hongera kaka Idd kwa kuchaguliwa tena, tuko pamoja nawe kama rais wetu kwa kipindi chengine, tunahitaji ushirikiano wa pamoja kuijenga DMV yetu kama ahadi zenu wagombea mulivyotuahidi kuwa dhamira yenu ni kuijenda DMV imara, uchaguzi umekwisha sasa tunataka kuona DMV iliyo imara
Mungu ibarikiDMV
Mungu wabariki watanzania