Kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam akionesha fedha bandia zilizokamatwa |
Jeshi la Polisi katika Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kukamata kundi la watu saba wanaotengeneza noti bandia za dola ya Kimarekani huko maeneo ya Sinza katika Hotel iitwayo Mombasa Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Watuhumiwa hao walikamatwa mnamo tarehe 04/8/2014 wakiwa na noti bandia zipatazo 10,640 za dola mia (100) ambazo ni sawa na dola 1,064,000 ambazo ni zaidi ya shilingi za Kitanzania bilioni moja katika
nyumba namba 07 walimokuwa wamepanga.
Polisi walipata taarifa kutoka kwa wananchi na kuweka mtego ambapo askari walifika katika eneo hilo na kuwatia mbaroni watuhumiwa wakiwa na noti hizo bandia zilizokuwa zimefungwa mabunda themanini na kasiki ndogo ambayo imefungwa kwa namba za siri.
Aidha watuhumiwa walikiri kujihusisha na utengenezaji wa noti bandia.
Watuhumiwa hao ni:-
1.AHMAD S/O MOHAMED Miaka 50, mfanyabiashara, mkazi wa Mombasa Kenya
2.RICHARD S/O MAGOTI Miaka 61, mfanyabiashara, mkazi wa Musoma mkoani Mara.
3.SIMONI S/O LUKIKO Miaka 58, mkazi wa Magomeni Kagera
4.HUMPHREY S/O LEONARD Miaka 34, mlinzi, mkazi wa Mburahati
5.FRANK S/O CHARLES Miaka 31 mfanyabiashara, mkazi wa Sinza
6.ABDALLAH S/O YUSUPH, Miaka 34, mfanyabiashara, Mkazi wa Sinza
7.BAKARI S/O BAKARI, Miaka 31, mfanyabiashara, mkazi wa Mbezi, Kimara.
Aidha watuhumiwa hao wanaendelea kuhojiwa na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.
2 comments:
Asante naomba sana muendeleze usakaji huo maana ziko nyingi saana hasa bongo magomeni na Kinondoni. Na hatua za kisheria zichukuliwe ipasavyo.
Unadhani ni zaki marekani tu ? Lazima wamefanya za nchi mbali mbali ikiwemo yetu.
sasa kama wanatengeneza zetu, je ni sawa ? Na inatuumizaje ki uchumi? Na kwani ni hao tu ? Na undhani kitu gani kilifanya wakamatwe ? Walimtuhumu mkuu gani ? Lazima wapo wengi wanafanya hivi na wanafadhali kwenye sehemu nyeti. Natabiri hili siyo tatizo geni na litaendelea tu kama vile ufisadi, uporaji kura, pa diem, mishara midogo, madawa ya kulevya, viroba, na matatizo mengi sugu. Sasa wadau angalia jinsi gani hili sakata litasahaulika tena haraka kwa sababu kuna viongozi wanaonufaika, kuna mapolisi wananufaika, na cha muhimu tulio wengi tutaumia tu. Ndiyo, si kodi itajapanda asilimia kadha ? Ehe. Sasa hili ni tatizo la nani? Kwa hakika kama jamii tusinyamaze, tukipiga kelele sana watasikiliza tu. Tukinyamaza kama ilivyo desturi wataendelea tu. Kumbuka wanaokamataa na wafadhili bado wanafaidi!
Post a Comment