TAMASHA la Usiku wa Matumaini, Dar (Dar Night of Hope 2014) lililofanyika jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar lilikuwa ni full msisimko kutokana na matukio mbalimbali yaliyofanyika.
Staa kutoka nchini Nigeria, Yemi Alade akipiga shoo usiku huu katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014 ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Yemi Alade akipiga shoo usiku huu katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014 ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Wakati mechi hiyo ilipokuwa ikikaribia kuanza, umati ulilipuka kwa shangwe baada ya kumuona Mfalme wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba alipokuwa alipoonekana akipasha misuli na wenzake.
Nyomi iliyokusanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar kwa ajili ya Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014.
BONGO MOVIES WACHEZA KIDUKULicha ya kufungwa, mashabiki wa Bongo Movies ndiyo walionesha kushangilia zaidi ya mashabiki wa Bongo Fleva ambao ndiyo walikuwa washindi.
Walicheza staili ya kiduku ile mbaya huku wakishangiliwa na umati uliofurika uwanjani hapo.
Bondia Mada Maugo amemshushia kichapo bondia Thomas Mashali katika mpambano wao kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014 ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar.
WABUNGE SIMBA VS YANGAWakati wa mechi ya wabunge, vituko ndiyo ilikuwa balaa. Kuna wakati baadhi ya waheshimiwa wabunge walikuwa wamechoka kiasi cha kushindwa kusogea lakini mwisho wa siku ilikuwa ni burudani kwani waliweza kubadilishana, wengine wakachukua nafasi. Hadi mtanange unamalizika, wabunge wa Yanga waliibuka kidededea kwa ushindi wa mabao 3 kwa 2.
Matukio mengine yaliyosisimua siku hiyo ni kama wasanii wa Bongo Fleva, Juma Nature, Shilole na wengineo ambao walipanda stejini kwa nyakati tofauti na kutoa burudani baab’kubwa.
Tamasha la Usiku wa Matumaini mwaka huu lilikuwa noma sana!
No comments:
Post a Comment