ANGALIA LIVE NEWS

Monday, August 11, 2014

UCHAGUZI WA DMV KASORO NYINGI ZILIJITOKEZA

Wasimamizi wakiendelea kuhakiki majina ya wapiga kura

Na Mwandishi wetu, DMV
Siku ya Jumamosi Aug 9, 2014 ndio siku ya wanaDMV walipopiga kura ya kuwachagua viongozi wao wapya baada ya malumbano na majitambo yaliyokuwepo kwenye mitandao ya kijamii na SMS za whatsup zaidi ya mwezi mmoja kila upande ukidai kuibuka mshindi.

Mvutano mkubwa ulikuwa kwenye kinyang'anyiro cha Urais kati ya mgombea Liberatus Mwang'ombe aliyebadilisha sura nzima ya uchaguzi huu na mgombea aliyekua anamaliza muda wake wa miaka miwili na kuamua kugombea tena kama katiba inavyoruhusu kwa kiongozi kukaa madarakani si zaidi ya miaka 4 kwa vipindi vya miaka miwili miwili.

Uchaguzi wa mwaka huu umechukua sura mpya kwa
mambo mengi ambayo hayakuwahi kujitokeza kwenye chaguzi zilizopita. Balozi wa Tanzania kupiga kura ni moja ya mambo mapya yaliyojitokeza kwenye kweye uchaguzi huu. Katika kumbukumbu za Jumuiya hii ya DMV tangia ilipoanzishwa miaka ya 80 Balozi hajawahi kupiga kura pamoja na kwamba yeye ndio anakuwa mlezi wa jumuiya. Ukiachilia mbali na hilo jambo lingine lililojitokeza ni wagombea kujinadi kwa wanavyuo kitu ambacho hakijawahi tokea katika chaguzi zilizopita, kingine ni wagombea kupita maofisini na majumbani na hata kufanya mikutano ya wazi kuomba kura na siku ya uchaguzi kufanya kila linalowezekana kuhakikisha mpiga kura wake amefika kituoni. Katika hili kuhakikisha mpiga kura aliyejiandikisha anafika kituo cha kupigia kura, timu Libe ilikua imejipanga vizuri zaidi na ilifanyakazi kama timu kwa kuweka usafiri kwa wapiga kura wao wasiokua na usafiri, pia waliweka watu nje ya jengo la kupigia kura na kujaribu kuwashawishi kumpigia kura mgombea wao kitu ambacho hakikuonekana kwa timu Iddi.

Ukija kwenye tume ya uchaguzi inaonyesha haikujipanga vizuri kukabiliana na mambo mengi yaliyojitokeza. Wakati kura zikipigwa, kuna makosa ambayo yangeweza kuepukika kama tume hiyo ingejipanga vizuri. Kila binadamu ana moyo na moyo unapopenda hua ni maradhi kwa maana kwamba kwa kamati kusimamia uchaguzi huu kwa wao kuwepo kwenye zile meza za kuhakiki wapiga kura Vijimambo inaona ilikuwa kosa kwa sababu inawezekana kwa msimamizi kuvunja utaratibu kwa sababu ya mapenzi na mgombea fulani.

Pili: muda uliowekwa kuanzia saa 8 mchana mpaka saa 4 usiku ulikua mrefu kwa mtu mmoja kusimama kwenye meza peke yake kwa saa zote, mwili wa binadamu kuusimamisha au kukaa sehemu moja takribani zaidi ya saa 9 husababisha akili kuchoka na kunaweza kuvuruga taratibu zilizowekwa.

Tatu: Uhakiki wa anuani ulikua ni tatizo kubwa tume ilichemsha sana kwenye swala hili pamoja na kwamba green card, pasi za kusafiria zinaweza kutumika kama kitambulisho lakini haziwezi kuonyesha mahali unakoishi na watu wanamna hii waliruhusiwa kupiga kura kwa utaratibu kwamba inabidi utambuliwe na wagombea. Vijimambo imeona hilo lilikua ni tatizo sehemu nyingi kinapotakiwa kitu kama hicho wanauliza uje na barua yenye jina lako inayoonyesha anuani unayoishi. Tume ingeweza kufanya hivyo pia kuhakikisha wanaokuja na pasi za kusafiria au green card waje na barua zenye majina yao zenye anuani za mahali wanapoishi ili kuepuka watu waliokuja toka nje ya DMV kutumia mwanya huo ili waweze kupiga kura.

Nne:Wasimamizi kwenye zile meza walitakiwa wawe watu toafauti kabisa asiyeishi DMV kama vili uchaguzi wa CCM DMV ulivyofanyika walileta msimamizi toka New York kwa ajili ya kusimamia uchaguzi huo kitu ambacho tume isingeshindwa kwa sababu ya DMV  inamahusian mazuri na majimbo mengine.

Mambo hayo hapo juu kama tume ingeyazingatia sidhani kama kungetokea msuguano huu uliopo sasa uliopelekea matokea ya urais kuchelewa kutangazwa, Jambo ambalo tume nasitahili sifa ni kuhakikisha ulinzi unakuwepo wa kutosha. Binadamu hujifunza kutokana na makosa ni matumaini yetu uchaguzi unaokuja tume itazingatia na kuzifanyia kazi kasoro hizo zilizotitokeza ili chaguzi zinazokuja zisiwe na matatizo hayo yaliyojitokeza kwenye uchaguzi huu,

Mwisho tunaipongeza tume ya uchaguzi kwa jitihada ilizofanya tangia mwanzo kuhusiana na uchaguzi huu tunajua ni kazi ngumu sana iliyohitaji hekma ya hali ya juu. Watanzania wenzangu uchaguzu umekwisha naomba tuwe kitu kimoja kama Watanzania asanteni kwa kunisoma,

1 comment:

Anonymous said...

Nilifikiri umekuja na a ngalau na suluhisho la maƱana. Kama uligundua tatizo kimsingi ni kurudia uchaguzi. Uchaguzi wa watu wachache chini ya 500 haukutakiwa huwe na kasoro nyingi Kama hizo. Uaminifu haukuwepo wa kutosha kwa wagawaji karatasi za kupiga kura. Pale ukumbini kulikuwa na Watu 430. Na absentee ballot 14 sasa nyingine 15 zilitoka wapi? Tume inakuwa kama monday quarterback . Wanakuja na majibu ya kipumbavu ya kuongeza idadi ya watu zaidi ya 430 waliohesabiwa. Suluhisho Kama mnataka mshikamano na imani kwa wanajumuiya na demokrasia ya kweli ni kurudia uchaguzi upya na usimamizi wa Kutosha. Na kabla ya kuweka kura yako ndani ya sanduku lazima ikaguliwe kuhakisha ni ONE MAN ONE VOTE.