Advertisements

Sunday, August 24, 2014

VIBAKA WAKAMATWA TABATA NA KUCHOMWA MOTO

 Baadhi ya wananchi wakishuhudia jinsi miili hiyo inavyoteketea.

Vijana wawili wakazi wa Jiji la Dar es Salaam ambao hawakufahamika majina yao, wanaodaiwa kuwa ni vibaka  alfajiri ya leo wameuawa kwa kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali baada ya kumpora pochi dada mmoja mkazi wa Tabata Liwiti. Shuhuda wa tukio hilo ambaye hakupenda kutaja jina lake alisema baada ya vibaka hao kumpora pochi dada huyo, walitaka kutoweka na bodaboda ndipo wananchi walifanikiwa kumkamata aliyeipora pochi hiyo akaanguka chini wakaanza kumpa kipigo huku mwenzake akifanikiwa kuondoka
 Matairi yaliyotumika kuwachomea vibaka hao yakiungua.

Miili hiyo ikiteketea kwa moto Kama waswahili wasemavyo za mwizi arobaini, kibaka huyo aliyekuwa akiendesha bodaboda kwa kasi, hakufika mbali pikipiki yake ikapata pancha naye akakamatwa na kuanza kupewa kichapo kisha walikusanywa pamoja wakavishwa matairi na kuchomwa moto.

Baada ya kuteketea kwa moto, polisi walifika eneo la tukio wakachukua mabaki ya miili ya vibaka hao na kuipeleka tatika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Crdt DJ Sek Blog

No comments: