ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, August 24, 2014

WANANCHI LUVUYO NA MBUNGE WAJENGA BARABARA YENYE THAMANI YA TSH MILIONI 52‏

Wananchi wa Kijiji cha Luvuyo Kata ya Madope wakimpokea Mbunge wao, Deo Filikunjombe kwa maandamano.
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na wananchi wa Kijiji cha Luvuyo kata ya Madope wakishirikiana jana na Deo Filikunjombe (kushoto) kuchimba mifereji ya maji katika barabara ya Luvuyo - Njombe yenye urefu wa Kilomita 6 ambayo inajengwa kwa ufadhili wa mbunge huyo kwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 50.
Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe akiwahutubia wananchi wa Luvuyo mara baada ya kuzindua ujenzi wa barabara ya Luvuyo - Njombe.
Deo Filikunjombe akisafirishwa katika mkokoteni wa kukokotwa na ng'ombe baada ya wananchi wa Luvuyo ambao awali walitishia kuhama wilaya ya Ludewa kuhamia Njombe kusikilizwa kilio chao cha ubovu wa miundombinu kwa kuanza kujengewa barabara na mbunge huyo.

Na Francis Godwin Blog
WANANCHI wa Kijiji cha Luvuyo, Kata ya Madilu wilaya ya Ludewa mkoani Njombe ambao awali walitaka kuhamia wilaya ya Njombe kutokana na Halmashauri ya wilaya ya Ludewa kuwatelekezea barabara ya Luvuyo – Njombe wamempongeza mbunge wao Deo Filikunjombe kwa kuwajengea barabara hiyo na kubadili uamuzi wao wa kuhamia Njombe.

Wakizungumzakatika hafla ya mbunge Filikunjombe kuzindua ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa zaidi ya 6 inayojengwa kwa zaidi ya milioni 52 ,walisema kuwa awali walipata kuandika barua katika uongozi wa Halmashauri hadi kwa waziri mkuu wakiomba kuhamia wilaya ya Njombe kutoka na kijji hicho kuwa kama kisiwa kutokana na ubovu wa barabara.

Mmoja kati ya wananchi hao Apudencia Lugome alisema kuwa wananchi hao walifikia hatua ya kuandika barua ya kutaka kijiji hicho kuwa sehemu ya wilaya ya Njombe kutokana na viongozi wa wilaya ya Ludewa kushindwa kuwatekelezea maombi yao ya ukarabati wa barabara ya kijiji hicho toka nchi ipate uhuru Kwani alisema kuwa mbali ya kujengwa kwa barabara ya Njombe – Ludewa ila wao katika kijiji hicho barabara hiyo ilikuwa si msaada kwao zaidi ya ile ya Luvuyo – Njombe ambayo hutumia kusafirisha mazao yao na ni tegemeo katika usafiri hivyo kitendo cha Halmashauri ya Ludewa kupuuza kilio chao ni kuwafanya wananchi hao kujisikia kama wapo katika kisiwa .

Hivyo alisema hatua kutoka na hali hiyo wao wenyewe wananchi walilazimika kuchangishana fedha kiasi cha Tsh 50,00 kila mmoja na kupata kiasi cha Tsh milioni 3.6 kwa ajili ya kuanza kutengeneza maeneo korofi kabla ya mbunge wao kufika katika mkutano wake na kuamua kuchukua jukumu ya kujitolea kujenga barabara hiyo yote .

“Tunashukuru sana mheshimiwa mbunge wetu na jembe kwa wana Ludewa kwani toka nchi yetu ipate uhuru Ludewa hatujapata kuwa na mbunge makini kama wewe hivyo hatuna sababu ya kuhangaika na mtu mwingine mwaka 2015….kwani mwenye kutatua kero zetu zaidi yako hakuna “

Huku diwani wa kata hiyo Godfrid Mhagama wa kata ya Madope akieleza kuwa sababu ya wananchi hao kufanya maandamano na kumpokea kwa usafiri wa ng’ombe ni kutokana na heshima kubwa ambayo mbunge huyo ameionyesha kwao wana kata ya Madope hasa wananchi wa kijiji cha Luvuyo.

Alisema kuwa barabara hiyo imekuwa kero kiasi cha wananchi hao kuwakimbiza watendaji wa Halmashauri ambao walifika katika kijiji hicho kwa ajili ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo.

“Kweli suala hili kwetu limetuumiza sana kichwa ilifika sehemu wakuu wa idara walikuwa hawafiki katika kijiji hiki kutokana na wananchi kuwa na jazba iliyotokana na ubovu wa miundo mbinu na ahadi zisizotekelezeka za Halmashauri yetu”

Katibu wa itikadi na uenezi CCM mkoa wa Njombe Onolatus Mgaya mbali ya kumpongeza mbunge huyo na wananchi kwa kuunganisha nguvu zao bado aliwataka wananchi hao kutunza barabara hiyo ambayo kukamilika kwake ni ukombozi mkubwa kwao.

Alisema kuwa wapo baadhi ya viongozi wamekuwa wakiangalia misaada inayotolewa na Mbunge huyo kwa macho matatu ambapo baadhi hujikuta wakiiba na kufanya ni mali yao binafsi kitu ambacho si kizuri bali wananchi washirikiane na viongozi hao kuhakikisha wanailinda na kuisimamia misaada wanayopewa iliiweze kuwanufaisha wote

“…Nampongeza sana Mbunge kwa misaada mbali mbali aliyotoa kwa wananchi wake kwani amejitahidi kuweza kutatua kero mbali mbali zinazowasumbua wananchi katika sekta ya afya, elimu ,m iundombinu na kilimo, naomba tuitunze na itumiwe na wananchi wote,"alisema Mgaya

Huku Filikunjombea mbali ya kuzindua ujenzi wa barabara hiyo pia alikabidhi msaada wa bati 200 ya geji 28 mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wwa nyumba ya mganga wa Zahanati ya Luvuyo na ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi katika shule za msingi kijijini hapo pia toroli na spendi kwa ajili ya kikundi cha vijana wanaojishughulisha na uoteshaji miti kijijini hapo bado aliwataka kuendeleza umoja zaidi .

Kwani alisema iwapo wananchi hao wataendelea kujitolea zaidi yeye kama mbunge wao atazidi kuwwaunga mkono na kuwahakikishia kuwa kamwe hatawaangusha katika utendaji kazi wake na kuwa siku zote anaamini kuwa mwwajiri wake ni mpiga kura na si vinginevyo.

" Ndugu zangu wana Luvuyo nawapenda sana baada ya kuja wiki iliyopita hapa na kufanya mkutano kweli nilivutiwa sana na jitihada zenu ndio maana nilikubali kuwasaidia kujenga badaraba hii kwa zaidi ya Tsh milioni 52 ila nawahakikishia fedha hizi hazijatoka mfukoni mwangu ila kutokana na kuishi na watu vema nimewaomba mitambo nja mafuta ya kuja kusaidia ujenzi huu baada ya kuvutika na jitihada zenu"

No comments: