Position ya kushika miguu inaitwa
Yogic treatment hii inaitwa Siddhasana
Yogic treatment hii inaitwa Dhanurasana
Zijuwe Faida
za Mazoezi ya Yoga
By: Sensei Rumadha Fundi
Kama mtaalam wa sanaa ya Yoga au Acharya (Yoga
Teacher), Rumadha (Rasadeva) alihitimu na kutunukiwa Diploma ya kufuzu sanaa
hiyo mwaka 1987, toka katika chuo cha "College
of Neohumanist Studies", Ydrefors,
Sweden, na hatimae baada ya kumaliza kozi hiyo kwenda Culcutta, India kwa
mafunzo maalum ya kuthibitiwa kama mwalimu wa sanaa hiyo. Pia Rumadha ni mwalimu
wa sanaa ya Karate. Mwaka 1991 alitunukiwa cheo cha juu cha sanaa ya Yoga
duniani kiitwacho " Avadhuta"
huko Calcutta, India chini ya kiongozi mkuu wa Yoga marehemu bwana "Shrii
Shrii Anandamurtiji"
Vitu vichache mwalimu Rumadha anapenda viongelea
kuhusu sayansi ya Yoga na uhusiano
kifikra na mawazo ya ubongo wa binaadamu.
Kutafakari "Meditation" au katika lugha ya Sanskrit "Dhyana"
mtiririko wa mawazo ni moja ya sehemu
kuu Yoga inasisitiza kuidumisha katika sanaa hii upanuzi.
Philosophy ya Yoga inaamini kwamba ubongo wa
mwanaadamu unatoa msisimko wa mawimbi ambayo huwasumbua sana binaadamu kuweza
kutumia uwezo wao wa fikra katika asilimia 100, na hatimae mwanaadam hutumia tu
asilimia 1, ya fikra zake na zote asilimia 99 hupotea kutikana na upungufu wa
utulivu wa mawazo ya mwanaadamu (
Concentration/ Focus).
Hivi karibuni tu, uvumbuzi mpya wa sayansi ya
Yoga amegundua kwamba ubongo wa mwanaadam umejengwa katika mchanganyiko wa
mabillion ya "Nervr Cells, hatimae kutoa mkondo mdogo wa umeme ( tiny electric current) ijulikanayo kama "Brain waves" ambayo hubadilika kila sekunde kufatana na mabadiliko
ya nguvu za ufahamu wako katika ubongo. Mashine yenye uwezo wa kuweza soma
mawimbi hayo ya ubongo hujulikana kama "EEG", au "Electroencephalogram" Chombo hiki kinapo fungwa kichwani
mwa binaadamu hutowa mawimbi na kuyasajiri kupitia mashine ya computer screen
na kutoa mawimbi yenye kina tofauti kutokana na nguvu za ubongo wa mtu.,
yaitwayo:
Beta Wave:
Mawimbi ya mizunguuko 13 kwa dakika ya ubongo
: kutokuwa na utulizu wa fikra'Stress/
Restless"
Alpha Wave:
Mawimbi ya mizunguko 8 kwa
dakika: msukumo imara kidogo wa
nguvu "Steady and rythmic
Amplitude".
Theta Wave:
Mawimbi ya 4 kwa dakika: Mawazo yenye nguvu za
ubongo, ubunifu na usanifu wa kisayansi ubongo umetulia.
Delta Wave:
Wimbi la 1
kwa dakika. Hapa nikupitia tu njia ya kutafakari ndio mtu huweza kufikia hatua
hii ya wimbi moja kwa dakika. Ubongo wenye nguvu zisizo kawaida " Intuitive mind/ subtler mind".
Moja ya gazi hii inauwezo wa kuwa utabiri wa
matokea ya mbele kutokana na upeo wa
fikra.
Lengo kuu la "Meditation" ni kuwa na uthibiti wa mawimbi ya ubongo kuweza
kupunguza kasi yake toke a mawimbi 13 kwa sekunde hadi wimbi
1 kwadakika na ubongo huo ndio upo katika watu wenye upeo wa fikra
zilizotulia kama maji ndani ya mtungi. Maji ya mtungi au kisima yakitulia ina
kuwa kama vile kioo, ukiangalia ujiona mwenyewe. Kama maji yakitibuliwa hutoawa
mawimbi mengi na kusababisha mvurugano nakutoweza kuona kimvuli chako mwenyewe au " Reflection."
Kupitia sauti itwayo "Matra", ubongo hutumia mbinu hiyo kama chombo cha kukufikisha
pale unakotaka kwenda. Pia Yoga ina masomo ya ngazi nyingi (Lessons).
Moja ya vitu sanaa Yoga inasaidia kuweza kumudu (Control) ya hisia zako mwilini yaani " Emotion", "propensities" kusaidia " Secretions of Hormones" kumudu hasira kupitia mazoezi yenye
utafiti wa kuiga mikao ya wanyama
kadhaa na ndege ambayo inaaminika wanatumia kwa kujitibu
wenyewe. bila kutumia dawa. Mikao yote ya Yoga (Yoga Postures) inasaidia matatizo kama vile:
Shindikizo la damu( High blood Pressure), uzito wa mwili ( Obesity), kisukari ( Diabetes)
na matatizo kadhaa ya magonjwa ya wanawake. Hivyo basi, Yoga ina faida nyingi
mno ambazo watu wengi hawazifahamu.
Yoga inaamini kwamba, kuna sehemu 7 za nguvu ndani ya mwili wa mwanaadamu kupitia uti wa
mgongo au "Kun'da'alini " katika lugha ya Sansrit ( Coiled Serpentine). Sehemu hizo ni :
1.Muladhara
Chakra: ipo katika mkia wa ya uti wa
mgongo 2. Sva'dhis;tha'na Chakra:ipo
sehemu ya kizazi (Groin area) 3. Man'ipu'ra
Chakra: ipo kitovuni. 4. Ana'hata
Chakra katika ya kifua. 5. Vishuddha
Chakra: ipo koromeo (Thyroid Gland) 6. A'jna
Chakra: ipo katikati ya macho (Pituitary). 7. Sahasra'ra Chakra: Ipo katika utosi.
Mwafunzi anapozidi kuendelea kwa kina katika
sanaa ya Yoga, ndipo anapo pita hizo sehemu ya nguvu 7 katika uti wa mgongo na
hatimaye kufikia hatua ya kuwa na udhibiti wa hizo hisia zake mwenyewe au "Propensities".
Sayansi ya Yoga nipana sana yenye kina kirefu na
filosofia yenye karne. Mazoezi ya Yoga husaidia viungo vya ndani ya mwili (Internal Organs) kama vile moyo,figo,
maini, kwa kuvikanda ( massage) zaidi
ya mwili wanje. Tofauti ya mazoezi ya gym na Yoga ki kwamba: Ukifanya mazoezi gym ( vigorous
exercise) unatumia sana nguvu na kuchoka haraka, wakati mazoezi ya Yoga ( Yoga Asanas) unalinda nguvu za mwili (Conserve Energy) hata kama na umri wa
uzee sana na kuwa umetulia (Relax). Yoga
ina njia yake ya tiba vilevile ijulikanayo kama: "Yogic treatment and remedies"
Hya ni machache tu kuhusu nini hasa faida ya
mazoezi ya yoga na mazoezi aina nyingineyo.
Sensei Rumadha pia ni mkufunzi wa sanaa ya Karate
mtindo wa "Okinawa Goju Ryu Jundokan Kyokai"
2 comments:
Kaka uko kamili sana tu Hongera sana ..
Hapo katikati ya macho...ndo nasikia third eye nguvu ya kuweza kuona vidivyoonekana kwa macho mawili ya kawaida...uchawi
Post a Comment