Advertisements

Wednesday, September 17, 2014

AIBUUU....NJEMBA NUSURA ITOLEWE JICHO BAADA YA KUCHEPUKA NA MKE WA MCHEZA (JUDO)

Mkazi wa Mtaa wa Lagos, Wazo Mivumoni, Msitu wa Pande jijini Dar es Salaam, Nuru Makala ‘Baba Eliza’ (42) Jumatano iliyopita alikumbwa na majanga baada ya mwanaume aliyejulikana kwa jina la Yusuf Ally ‘Mgosi wa Ndima’ kudai amemfumania Baba Eliza akiwa na mkewe ambaye jina halikupatikana.

Tafrani hiyo ilijiri usiku wa Jumatano iliyopita, Juni 18, mwaka huu kwenye nyumba yake iliyopo Mtaa wa Lagos, Msitu wa Pande. 
Akizungumzia tukio hilo mbele ya wanahabari waliokuwa eneo hilo wakisaka habari, Yusuf Ally ambaye ni mume wa mwanamke aliyefumaniwa alisema: 

“Nilikuwa katika harakati za kumchunguza mke wangu kinyemela kwa siku nyingi kama anachepuka, nikabaini kuna mawasiliano yenye shaka kati yake na huyo jirani yangu. 

“Nilipomuuliza mke wangu alikiri, akasema amekuwa akimwambia jirani yangu kwamba haiwezekani lakini jamaa anakomaa tu anamwambia wakutane, tena wakutane humu ndani. 

“Ndipo nilipoamua kumuandaa mke wangu kwa mtego amwambie jamaa kuwa leo (siku ya tukio) sitakuwepo na sitarudi ili kumpa nafasi jamaa kuja kujinafasi. Baada ya kukamilisha mtego niliwasiliana na kamanda wa sungusungu wa eneo hilo, Kapteni Makumba na kumuelezea kinagaubaga. 

“Kapteni Makumba aliwaandaa vijana wake ambapo kuanzia mishale ya saa mbili usiku walijibanza kwenye kichaka kilichopo mbele ya nyumba huku akifanya mawasiliano na mimi.”
Mgoni akiomba Msamaha.

Yusuf aliendelea kudai kuwa, ilipotimu saa tano usiku kukiwa kumetulia, Baba Eliza alionekana akikaribia nyumba ya jirani yake huyo kwa hatua za kunyata na kuangalia kulia na kushoto kisha akazama ndani huku mkononi akiwa ameshika kifurushi kilichobainika baadaye kwamba kilikuwa na machungwa kadhaa. 

Alisema muda mfupi baada ya kuingia, sungusungu mmoja alikwenda kujibanza kwenye dirisha la chumba na kupiga chabo kilichokuwa kikiendelea ambapo alimshuhudia Baba Eliza akichojoa nguo chapchapu tayari kwa mtanange, sungusungu huyo akawatonya wenzake. 

Yusuf akazidi kusema kwamba wote walitoka kichakani na kwenda kuvamia chumbani ambapo walimkuta mkewe aliyekuwa bado hajaanza kuvua nguo kwa sababu alijua majanga yatatokea muda si mrefu akiwa anajiandaa kufanya hivyo kiaina.
Baada ya hali kuwa shwari, Kamanda wa Sungusungu, Kapteni Makumba alianza kumsomea mashitaka jirani huyo aliyekuwa mtupu muda huo mbaye hakuwa na la kusema zaidi ya kuomba radhi na kumtupia lawama ibilisi kwamba ndiye aliyemshawishi na haikuwa amri yake. 
Raia aliyeshuhudia mkasa huo akionesha sehemu ya kitanda iliyochafuliwa na mgoni kwa kinyesi. 

Sungusungu walimtaka Baba Eliza kumlipa fidia ya shilingi milioni moja mwenye mke kwa kitendo cha kumdhalilishia ndoa yake.

No comments: