Advertisements

Friday, September 5, 2014

AJALI MBAYA YATOKEA MUSOMA ZAIDI YA WATU 30 WAMEFARIKI DUNIA

Mabasi hayo yakiwa yamegongana

Basi la Jumanne lililokuwa linatoka Sirari kwenda Mwanza limegongana uso kwa uso na basi la Mwanza coach lililokuwa linatoka Mwanza kwenda Musoma. Ajali imetokea katika eneo la daraja la sabasaba, Musoma. 
Maelezo kwa Mujibu wa Father Kidevu blog

6 comments:

Anonymous said...

KILA SIKU NI AJALI..AJALI...AJALI MPAKA LINI? AU NDIYO NJIA YA KUWAPUNGUZA WATANZANIA NA KUONGEZA IDADI YA WALEMAVU WASIOSAIDIWA CHOCHOTE NA SERIKALI YETU? KWANINI TUSIIGE NCHI ZILIZOENDELEA KWENYE UDHIBITI WA MADEREVA NA KUWATIA ADABU WALE WOTE WANAOFANYA UPUMBAVU NA KUWEKA VIFUNGO VIREFU ILI IWE FUNDISHO KWA WANAOZEMBEA? LEO WAMEKUFA WATANZANIA WASIO NA HATIA 35 NA WENGINE WAMEKUWA MAJERUHI SANA WENGINE WAMEKATIKA MIGUU, UJUE HAO WALIOKATIKA MIGUU, MIKONO AU VIUNGO VINGINE WALIKUWA WAZIMA JANA TU SASA NANI ATAWATUNZA? SERIKALI? MISIKITI AU MAKANISA? SIDHANI KAMA KUNA MMOJA KATI YA HAO ATAWATUNZA? WATABAKIA MASKINI MAISHA YAO YOTE KWA AJILI TU YA SERIKALI (POLISI) KUACHA SEKTA YA USAFIRI IJIONGOZE KIHUNI HUNI NA POLISI WAJICHUKULIE RUSHWA KANA KWAMBA HAWALIPWI. SERIKALI YETU IMELALA SIKU ZOTE NA SIDHANI KAMA ITAAMKA SASA HIVI. KESHO UTAONA KWENYE BLOG HII TAARIFA YA SERIKALI KUWA RAIS AMETUMA RAMBIRAMBI NA AMESIKITISHWA SANA NA WATANZANIA KUFA. HAPO HAWAJAANGALIA UBOVU, UFINYU WA BARABARA NA ULIO CHINI YA VIWANGO, BARABARA ZETU HAZINA WARNING (ILANI) YA KUONYESHA DARAJA AU SEHEMU YA HATARI NA VIWANGO VYA MWENDO UNAOTAKIWA KUENDESHA KWENYE SEHEMU TOFAUTI.
SIJAWAHI ONA MAGARI YAMEGONGANA NA KUHARIBIKA KIASI HIKI....HIVI HUO MWENDOKASI(SPEED) UMERUHUSIWA NA NANI? POLISI...SERIKALI...SUMATRA AU?
TUNASUBIRI RAMBIRAMBI KUTOKA KWA RAIS KUTUAMBIA AMESIKITISHWA SANA LAKINI HAKUNA HATUA ZA KUCHUKULIWA KWA SABABU TUMEZOEA KUFANYA KAZI TUNAVYOJUA.....HAKUNA CREATIVITY. BAADA YA WIKI MOJA UTASIKIA AJALI NYINGINE MBEYA, MOSHI, IRINGA AU DODOMA....MTINDO WETU ULE ULE....RAIS AMESIKITISHWA SANA!!! UFUMBUZI------HAKUNA! BAADA YA MUDA NCHI YETU ITAJAA WALEMAVU WALIOPATA AJALI KWA MAKOSA YASIYO YAO.

Anonymous said...

Udhibiti uende sambamba na kuwaondoa madreva wajinga kwenye usukani. Yaani huyu dreva kajiua mwenyewe na roho za watu zaidi ya 30, kisa? Anataka kuwahi kuvuka daraja. Sasa amewahi?
Haya mambo yapo sana Tanzania. Usiombe ukutane/upande basi linalotoka Geita, Bukoba na wilaya zake. Madreva wanaenda speed ya ajabu eti wanawahi kivuko. Yaani nchi haina wabunifu hata kidogo. Rais sasa hivi anawaza safari yake nchini Marekani.
Kama unabisha angalia swala la katiba. Hawa jamaa wameteka kila kitu. Yaani bora iliyopo kuliko wanayotaka kutupa. Kibaya zaidi, wote waliapishwa kabla ya kuanza kazi. Sasa utategemea polisi, mahakama, Rais kulinda chombo ambacho waandaaji hawakukilinda?
Tunaandaa taifa si la walemavu wa miili tu bali wenye macho ila vipofu, wasioweza kufikilia kabisa. Mimi huwa natamani mkoloni arudi.
Watu wanafikilia kwa matumbo tu. Hivi umeongea na mtu anayejiita engineer tanzania? Atakwambia ana kampuni ya ujenzi na kila kitu. Mpe kazi uone. Hata kama hawezi atachukua tu. Anaweza kuwa na tenda kama 100 lakini bado yumo. Kitu cha laki moja, atakucharge laki mbili.....sasa ukiingia ubora wa vitu anavyotengeneza ndo utalia. Yani sio wabunifu kabisa. Kucopy na kupaste nyumba za watu afu customer service yao ni zero kabisa. Yaani kama viongozi wetu.
Watanzania wenyewe si unaona wanavyoteseka? Ngoja ifike mwaka kesho. Kama umezaliwa leo, unaweza kudhani hawa watu wameteseka sana hivyo watafanya mabadiriko. Yaani utawanunua wote kwa kutenge na kofia. Utatuma malori kuwakusanya kwenye mikutano yako na watajaa wakushangilie. Uchaguzi ukiisha, oh, serikali, hamna sheria! Utadhani sio hao ulonunua. Pengine ngoja wateseke, wafe. Labda siku moja wataamka usingizini. Huwezi kumwonea huruma mtu asiejihurumia.

Anonymous said...

Nakubaliana na mdau hapo juu 100% , hii inanifanya nichukie nchi kabisa, kila kukicha ni ajali kwa ajili ya uzembe, tanzania tunaelekea pabaya sana kwakweli, so sad, R.I.P

Anonymous said...

Kuna msemo wa Kiswahili wa kijinga unasema, "Ajali haina kinga"!!!!

Anonymous said...

Kazi ipo! Jumala kuu ni kwamba mwenye kutekeleza sheria hataki kuwajibika kwa sababi pengine ni bugudha na pia mfuko wake wa hela chezea utaondoka. Hivyo nasema tamaa ya pesa na mali mbali kwa njia zakulazimishia zina maaliza wananchi yetu. Sasa tunachanga moto ndugu zangu. Tuendelee kulala, tuendelee kunung'nunikia, tuendelee laani kwa upole sana na kusikitika....kama iliyokwaida, siyo. Au tuamke! Tunauwezo wa kusaidiana. Tena kwa amani. Dereva akishajulikana mbaya, mkorofi wasafiri pigeni picha. Tumeni kwenye mtandao, ipi mingi. Shikeni number za gari na jina lake yeye na konda, na kampuni. Watuwakiion hizo sura wataamua kutokopanda basi na itanusuru maisha wengine. Kama kampuni lina madereva bovu kila leo itajulikana tu. Maisha ya watu yatanusurika. Huu ni mchango wangu, maana bado tunao uwezo na option yakuelemishana na uamuzi wa kutokupanda mabasi na kuendeshwa na madereva wauaji. Tuone kama hili halitaanza kusaidia! Ni zoezi la ushirikiano, hali hii hitaju polisi, halaumu serikali na litaokoa watu. Je uncle unaweza kutusaidia na hili zoezi? Je wadau tunaweza kushirikiana na kutokomeza ujinga huu ? Asanteni

Anonymous said...

AJALI ZA KIZEMBE NCHINI TANZANIA

Dr. Mwakyembe, tunashuku kwa gesture nzuri uliyoionyesha kufuatia ajali ya kusikitisha, kizembe na ya kuepukika kwa 100% iliyotikisa taifa letu na hata tunaokaa nje ya nchi! Dr. Mwakyembe amelitumikia taifa letu kwa uzalendo na uaminifu mkuu. Lakini napenda nimkumbushe Dr. Mwakyembe kuwa uzembe huu wa kupoteza watu kwa ajali za kuepukika haujaanza jana, wala juzi. In fact, ni tatizo sugu ambalo Dr. Mwakyembe alilikuta na hajafanya juhudi za kutosha, angalau basi hata kulipunguza na vigumu kusema kuwa yeye si sehemu ya tatizo! Nasikitika kusema kuwa hizi ajali hazitaisha mpaka uongozi na Tanzania kama nchi, itakapothamini na kutambua kuwa hata roho moja ikipotea kwa uzembe ni pigo kwa taifa.

Mwisho, ningemsihi Dr. Mwakyembe kwenda hatua moja zaidi, mbali tu ya kuyafungia magari leseni za usafirishaji. Uaji magari kwasababu ya uzembe,  inabidi iwe categorized as a felony au crime and is punishable to the fullest extent of the law, including kufungia leseni ya kuendesha. Pili, ahakikishe kuwa hizo kampuni zilizofungiwa hazitumii loophole au ujanja wa kubadilisha majina ya biashara, kuuzia ndugu ili kurudi tena barabarani kwa majina mengine.