Rais Jakaya Kikwete amesema moja ya vyanzo vikubwa vya kuzalisha, kulea na kukuza ugaidi duniani ni sera mbaya za ubaguzi na zinazowanyima haki za msingi baadhi ya wanajamii ama makundi ya wanajamii.
Pia amesema ni muhimu kwa mataifa mbalimbali duniani kubuni na kutunga sera, ambazo zinalenga kutoa nafasi na haki za msingi kwa kila mwanajamii na mwananchi kufurahia sehemu ya keki ya taifa.
Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, jijini Dar es Salaam, ilitumwa kwa vyombo vya habari jana ilimkariri Rais Kikwete akisema sera za kiuchumi na kijamii zina mchango mkubwa katika kukabiliana na kupambana dhidi ya ugaidi na vitendo vya msimamo mkali wenye kutumia nguvu na fujo katika nchi yoyote.
Rais Kikwete alisema hayo jana, alipozungumza katika mkutano wa Wakuu wa Nchi za Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika kwenye kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Kenyatta, jijini Nairobi, Kenya chini ya uenyekiti wa Rais Idrisa Debby wa Chad.
Katika mchango wake kwenye mkutano huo, Rais Kikwete alisema ni dhahiri kuwa ugaidi ni tishio la kweli la Bara la Afrika kwa mujibu wa ripoti iliyowasilishwa kwenye mkutano huo na Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU, ambayo ilielezea kwa uwazi tishio la ugaidi.
“Kwa kuongozwa na ripoti hii, tunatambua sasa kuwa ugaidi ni tatizo gumu sana kwa sababu hakuna nchi duniani isiyoguswa nao na hakuna nchi hata moja duniani yenye uwezo wa kukabiliana nao peke yake. Hivyo, ni muhimu kuunganisha juhudi zetu kwenye ngazi zote; ngazi ya kitaifa, kikanda, kibara na duniani ili kuweza kukabiliana nao ipasavyo,” alisema Rais Kikwete.
Aliongeza: “Kuna maswali mawili muhimu ambayo tunastahili kujiuliza na kuweza kupata majibu mwafaka juu ya kwa nini kuna balaa la ugaidi na jinsi gani tunavyoweza kukabiliana nalo.
Katika jitihada zaidi za kukabiliana na tatizo hili ni lazima tutafute kiini hasa cha kujaribu kumaliza ugaidi na vitendo vya msimamo mkali wa kutumia nguvu na fujo. Katika hali hii, sera za kiuchumi na kijamii katika kila nchi zina mchango mkubwa katika mapambano haya.”
Hata hivyo, alisema wakati mwingine ugaidi unaweza usiwe na mazingira ya kuzaliwa ndani ya nchi kama ilivyoonekana wakati balozi za Marekani jijini Dar es Salaam na Nairobi zilipolipuliwa kwa mabomu.
“Kikundi cha Al-Qaeda kilikuwa na matatizo na Marekani na kikaamua kuzifanya Tanzania na Kenya uwanja wa mapambano,” alisema Rais Kikwete.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment