Baada ya kutoa elimu juu ya mafanikio na ujuzi wa biashara na ujasiriamali kwa wanawake wajasiriamali mkoani Mwanza, kampeni ya mwanamke na uchumi inahamia mkoani Tanga ambapo wanawake na vijana zaidi ya 600 wanategemea kupata elimu ya msingi juu ya ujasiliamali na fursa zilizopo na nidhamu ya matumizi katika kuhifadhi fedha na mikopo.
“Sasa tunahamia mkoa wa Tanga ambapo sasa mafanikio ya kampeni ya mwanamke na uchumi tunayapeleka kwa wanawake wajasiliamali na vijana ambapo pamoja na mambo mengine,
tumefanya tathimini ya mkoa wa Mwanza imeonesha mafanikio makubwa kwani mrejesho ni mkubwa na hamasa ni ya kutosha ambapo wajasiriamali wanatuomba turudi tena, na hili ni jambo la kutia moyo”Anasema Naima Malima Mkurugenzi wa Angels Moment waratibu wa kampeni ya mwanamke na uchumi kwa wanawake wajasiriamali nchini.
“Unajua mkoa wa Tanga unafursa nyingi sana,na jambo la kufurahisha ni kwamba viongozi wengi wa mkoa huu ni wanawake kama mimi, ukianzia mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya wote ni wanawake na wanajitahidi kuhakikisha wajasiliamali wanasonga mbele ambapo pamoja na mambo mengine masuala haya yatajadiliwa na kufundishwa na wataalamu na watoa mada hivyo elimu ya ujasiliamali na fursa zilizopo, usimamizi binafsi wa fedha na uwekaji akiba,
afya bora na uchumi kwa akina mama na mwisho ni mwanamke na rslimali ardhi tunategemea mada hizi zitafundishwa kwa usitaadi wa hali ya juu na wakufunzi wetu” anasisitiza Mkurugenzi huyo.
Kampeni ya mwanamke na uchumi mkoani Tanga inatazamiwa kuhudhuliwa na wawezeshaji na wakufunzi maarufu kama ndugu Emiliani Busara na Bi.
Tabu Likoko kutoka taasisi ya WAMA ya jijini Dar es Salaam. Elimu sahihi juu ya mada tajwa hapo juu zitatolewa ambapo wanawake wajasiriamali kutoka wilaya za Tanga, Muheza, Mkinga na Pangani zitashiriki.
Kampeni hii ni ya pili kufanyika katika mkoa wa Tanga,baada ya awali kufanyika mkoani Mwanza ambapo itapambwa na Balozi wa kampeni ya mwanamke na uchumi Mwanamziki LINAH SANGA ambaye ataburudisha na kutoa elimu kupitia mziki wake na wimbo maalumu wa kampeni ya mwanamke na uchumi ambapo imepanga kufanyika terehe 10 na 11 mwezi ujao jijini Tanga.
No comments:
Post a Comment