ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, September 10, 2014

KWA STAILI HII TUTAENDELEA KUFA KWA MAPENZI YA MUNGU

Mbeya yetu iliwashuhudia Abiria hawa bila Kujali hatari wakiwa wanajipanga kupanda katika Gari la Mizigo huku kukiwa na usafiri wa usalama na wakutosha kabisa. Wakina mama wengine walikuwa na Watoto wao bila kujali afya zao kwa kuwa barabara hiyo ilikuwa na vumbi la kutosha.
Askari wa usalama barabarani akiwa kazini
Askari wa usalama barabarani akitumia mamlaka yake kulisimamisha Gari lililoshehena Mizigo na Abiria Juu
Hata hivyo uchunguzi umebaini Bajaji kubeba abiria ili kulisubiria Lori mbele kama inavyo onekana Pichani.
Cha Kushangaza zaidi hakuna abiria aliyeshushwa wala mizigo na kuamriwa kuendelea na Safari , Je hapa tuseme ni usalama wa barabarani au ni Hatari barabarani 
Kwa Furaha Abiria walioshushwa na Bajaji wakisubiri Lori kwa matumaini ili kuendelea na Safari yao.
Safari inaendelea bila wasi wasi kila Lori na Safari yake na kwa nafasi
Mizigo Imesheena na abiria wamesheena
Safari inaendelea bila wasi wasi ambapo Tulibaini kwa ukaribu kabisa Gari la kwanza la Mizigo likipita Ishara kuonesha kuwa liliruhusiwa pasipo na Pingamizi
Lori la pili nalo linapita nalo bila wasiwasi , Tazama hapo juu huyo abiria wa mbele alivyo jiegesha je Kuna tahadhari yotote hapa? Hapa pia tulibaini Askari wa usalama wa barabarani aliliruhusu bila kipingamizi
Na Hatimaye huku mbele tukashuhudia Mistubishi ambayo tuliiona ikiwa imesimamishwa na Askari wa usalama wa Barabarani nayo ikipita tena ikiwa na watu wengi ndani yake mpaka wengine hawajakaa  vizuri kama wanavyo onekana a


WAKATI Serikali na wadau mbali mbali nchini wakihaha kuepusha ajali zinazoendelea kuangamiza roho za watu, hali imekuwa tofauti kwa baadhi ya madereva na wamiliki wa vyombo vya usafiri.
 
Ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani umejitokeza mara nyingi Barabara za Mbeya-Chunya kupitia Kawetele na Mbeya-Mkwajuni Kupitia Mbalizi ambapo yamekuwa yakibeba abiria na mizigo licha ya kuwepo mabasi yaliyoruhusiwa Kisheria.

 Mbeya yetu imeshuhudia  magari matatu aina ya Fuso na Scania kubeba mizigo na kuning’iniza abiria juu jambo linalohatarisha usalama wa abiria na mali zao.
 
Magari hayo yalikutwa hivi karibuni  yakitokea jijini Mbeya na kuelekea Wilayani Chunya majira ya saa Tisa alasiri huku wasimamizi wa sheria za usalama barabarani na Sumatra wakiyaruhusu kuendelea na safari licha ya kuyaona yakifanya safari zake kila siku.
 
Mbeya yetu ilishuhudia magari hayo yenye namba za usajili T 168AZG aina ya Fuso, T 432 AAK aina ya Scania na T 646 BRQ aina ya Mitsubishi Fuso yakiwa yanapita barabarani eneo la Mwansekwa na kuyashuhudia yakipita Lwanjiro kwa ishara kuwa yaliruhusiwa kuendelea na safari.

Hata hivyo usalama wa abiria hao umekuwa mashakani licha ya Serikali kuimarisha barabara ya Mbeya-Chunya na kuwepo kwa magari ya abiria Lukuki yanayofanya safari zake kila siku na Sumatra kuamua kupunguza Gharama za usafiri. Ambapo awali walikuwa wakitozwa Tsh 10,000 kati ya Mbeya na Chunya na sasa nauli imefikia hadi Tsh 5,000. 
 
Hali hii Hatari huwa mbaya zaidi wakati wa minada inayofanyika maeneo mbalimbali katika Wilaya ya Chunya na Magari hiyo yamekuwa yakipita pembezoni mwa kituo cha Polisi cha Wilaya hiyo.


MBEYA INAULIZA JE WAHUSIKA MNALIONA HILI? NA TAMKO TUNANGOJA LITOLEWE HADI WAKATI WA MAAFA?

NDUGU MDAU KARIBU KUCHANGIA MAONI.

NA MBEYA YETU BLOG.

4 comments:

Anonymous said...

Na askari anaangalia tu!

Anonymous said...

Asanteni sana MBY yetu kwa kutujuza kwa picha. Je ndugu mdau na mwandishi wa MBY yetu umewahi jiuliza swali hili kwanini jeshi la DRC lilishindwa dhidi ya M23, nao Nigeria kushindwa na BOKO haramu? Jibu lako litakuelekeza kwa trafic police wa tz. Hata uunde tume ni bure kwa nyakati za sasa. JWTZ waliwamaliza M23 na maswala ya barabarani nayo tutayamaliza kwa kuwaleta askari wa nje sababu sisi rushwa ni life style. Watu wetu wataendelea kufa kila leo. Hata watu wetu nao they need civic education. Mdau wa DC USA.

Anonymous said...

Wajameni Tatizo hili ni la kimifumo na Utekelezaji mbovu wa viongozi wetu pamoja na UKOSEFU WA CHECK AND BALANCE. Kwa mfano, habari kama hii inayoambatana na picha ni ushahidi tosha wa matatizo wa polisi katika kusimamia sheria. Swali kamanda wa polisi wa mkoa/wilaya wanafanya nini katika hili. Huyu kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya anakawaida ya kutoa taarifa kila mwezi je haoni umuhimu wa kutupa taarifa ya ni nini amekifanya baada ya tukio kama hili la kizembe? Badala ya kungojea ajali zitokee na kuturipotia watu waliokufa na kujeruhiwa?

Anonymous said...

Tatizo ninavyoona ni hakuna mabasi kama kungekuwa na mabasi watu wasingepanda malori