Advertisements

Wednesday, September 10, 2014

MAMA WA FEZA NUSURA AUAWE

Mshiriki wa shindano la Big Brother Africa, Feza Kessy.
Stori: Mwandishi Wetu
WAKATI hofu ya mauaji ya wanawake ikiwa bado imetanda mkoani Arusha, mama mzazi wa mshiriki wa shindano la Big Brother Africa, Feza Kessy ameponea chupuchupu baada ya kuvamiwa na majambazi wawili kisha kuporwa fedha.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu kutoka jijini humo, Feza alisema mama yake aitwaye Rose Kessy alikutwa na masaibu hayo mchana wa saa nane, Jumatano iliyopita akiwa hatua chache kutoka nyumbani kwake, eneo la Boma ya Siara, Moshono.

“Watu wawili wakiwa na pikipiki walimsimamisha akiwa garini anarejea nyumbani, wakamteremsha na kuanza kumsachi, wakachukua pochi yake ambayo ilikuwa na shilingi laki tatu ndani. Wakati wanafanya tukio hilo watu walikuwa wanatazama tu bila kufanya lolote.

“Watu wengine walipita na gari wakataka kusimama, lakini wakaonyeshwa bastola na kupewa ishara ya kuendelea na safari. Yaani walikuwa wanafanya wakiwa hawana wasiwasi utafikiri ni askari vile, hivi hapa ndiyo nimerudi kutoka polisi,” alisema mshiriki huyo ambaye pia aliwahi kushiriki shindano la Miss Tanzania miaka ya nyuma.
Alisema wakati wa tukio hilo, mama huyo anayefanya kazi Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita wa Rwanda (ICTR) alikuwa ameambatana na mtoto wa msanii huyo wa Bongo Fleva, aitwaye Jayden mwenye umri wa miaka mitano.Alisema baada ya majambazi hao kuondoka, Polisi walifika nyumbani kwao kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Credit:GPL

2 comments:

Anonymous said...

Arusha kunaongopesha

Anonymous said...

mkome hiyo misifa yenu ya kujitangaza mnapesa mko famous etc ndo maana mijambazi inakungiliyeni na kuja kukuporeni kwa misifa yenu ya kipumbavu pumbavu ya kujitangaza tangaza kila leo mna hichi na kila na pesa hivi na vile.
kwani mkikaa kimya inakuwaje mnakosa nini wangapi wako na pesa mbona wako kawaida na kujichanganya na watu maskini ile mbaya.