Meriam Ibrahim kushoto na Papa Francis
Mwanamke raia wa Sudan ambaye alihukumiwa kifo mapema mwaka huu kwa kuikana dini ya kiislamu ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu awasili nchini Marekani mwezi Julai.
Meriam Ibrahim alipokea tuzo kutoka kwa shirika moja la kikristo mjini Washington lililomtunuku kwa ujasiri wake.
Kwenye mahojiano na BBC Meriam alisema kuwa kile anachotaka kufanya ni kuendesha kampeni kwa niaba ya wale wote wanaokabiliwa na mauaji ya kidini.
Alihukumiwa kifo akiwa mja mzito na mahakama nchini Sudan kwa kuasi dini yake.
Kesi hiyo ilizua shtuma kali kote ulimwenguni.Bi Meriam alizaliwa na baba mwislamu lakini akalelewa kikristo na mamaake.
lakini chini ya sheria za Sudan mahakama hiyo haikutambua dini wala ndoa yake.
Alitakiwa kubadili dini ama auawe.Akiwa amehukumiwa kifo alijifungua mwanawe ndani ya jela,ambaye aliishi naye katika eneo hilo kwa mda.
Hatahivyo kampeni ya kimataifa ya kuitaka serikali ya Sudan kumwachilia huru ilianzishwa na kusababisha kuachiliwa kwake.
CREDIT:BBC
2 comments:
Mchumia tumbo na msaka tonge,dunia inakuumbua na kukucheza shere usiyejijua.
Basi hapo ndipo mlipokosea. Baba yake alikuwa muislamu, akaoa mke wa kikristo lakini hakumsilimisha. Mtoto alipozaliwa mama yake akawa anampeleka kanisani, baba yake hakulalamika. Huyu hajakana dini. Amekulia kwenye dini ya ukristo kwa ridhaa ya wazazi wake wote. Upo hapo? hiyo ndo hali halisi.
Post a Comment