Kikosi cha Young Africans kilichoanza leo dhidi ya Tanzania Prisons
Mabingwa mara 24 wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Young Africans leo imeipata ushindi wake wa kwanza kwenye VPL baada ya kuichapa timu ya maafande wa jeshi la Magereza nchini Prisons kwa mabao 2- 0 kwenye dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kikosi cha mbrazil Marcio Maximo kiliingia uwanjani kwa lengo la kusaka pointi muhimu kutokana na kuwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wake wa ufunguzi dhidi ya wakata Miwa wa Mtibwa Sugar mjini Morogoro mwishoni mwa wiki.
Young Africans iliuanza mchezo kwa kasi na kufanya mashambulizi kadhaa langoni mwa Prisons kupitia kwa washambuliaji wake Jaja, Coutinho, Ngasa ambao waliokua wakisaidiwa na na viungo Hasssan Dilunga na Haruna Niyonzima lakini kutokua makini kwa washambuliaji hao kulifanya kutopata bao la mapema.
Dakika ya 34 ya mchezo, mshambuliaji raia wa brazil Andrey Coutinho aliwainua vitini washabiki wa Young Africans baada ya kuipatia timu yake bao la kwanza kwa mpira wa adhabu alioupiga na kujaa wavuni moja kwa moja kufuatia Mrisho Ngasa kuchezewa madhambi nje kidogo ya eneo la hatari.
Kiungo wa Prisons Jacob Mwakalobo alitolewa nje kwa kadi nyekundu na mwamuzi wa Andrew Shamba baada ya kumchezea madhambi Mrisho Ngasa ikiwa ni kadi ya pili ya njano baada ya kuwa tayari alishampatia kadi ya njano kwa kumchezea Jaja.
Mara baada ya bao hilo, watoto wa Jangwani waliendelea kulisakama lango la Prsions kwa lengo la kuongeza bao la pili lakini kutokua makini kwa washambuliaji wake kulipelekea kwenda mapumziko Yanga wakiwa mbele kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa mabadiliko ambapo Young Africans iliwaingiza Saimon Msuva na Hamis Thabit kuchukua nafasi za Andrey Coutinho na Hassan Dilunga mabadiliko ambayo yaliepelekea kuongeza kasi ya mashambulizi.
Dakika ya 65 mshambuliaji wa Prisons aliyeingia kipindi cha pili Ibrahim Kahaka aliipatia timu yake bao la kusawazisha kwa kichwa kufuatia krosi nzuri iliyopigwa upande wa kulia na kumkuta mfungaji aliyewazidi ujanja walinzi wa Young Africans pamoja na mlinda mlango Deo Munish "Dida" na mpira kujaa wavuni.
Saimon Msuva aliihakikishia Young Africans ushindi katika mchezo wa leo baada ya kuipatia timu yake bao la pili dakika ya 68 ya mchezo kwa kichwa akimalizia krosi safi iliyopigwa kutoka winga ya kulia na Mrisho Ngasa na kumkuta mfungaji Msuva ambaye hakufanya ajizi.
Baada ya bao hilo vijana wa Magereza kutoka Mbeya walicharuka kusaka bao la kusawazisha kwa kufanya mashambulizi mfululizo langoni mwa timu ya Young Africans lakini umakini wa walinzi wake na mlinda mlango vilipelekea dakika 90 kumalizika 2-1.
Young Africans: 1. Deo Munish "Dida", 2. Juma Abdul, 3.Edward Charles, 4. Nadir Haroub "Cananavao" (C), 5.Kelvin Yondani/Rajab Zahir, 6.Mbuyu Twite 7.Hassan Dilunga/Hamis Thabit, 8.Haruna Niyonzima 9.Geilson Santos "Jaja" 10.Mrisho Ngasa, 11.Andrey Coutinho/Saimon Msuva
No comments:
Post a Comment