Mwenyekiti wa BAWACHA ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Kawe kupitia CHADEMA Halima Mdee akiwa katika maandamano akiwaongoza wanawake wenzake kuelekea Ikulu kumpelekea ujumbe Rais Jakaya Kikwete kwamba hasikubali kuweka saini Rasimu mpya iliyopitishwa juzi mjini Dodoma, maandamano hayo kabla hayajafika mbali walitawanywa na jeshi la polisi lililotumia maji ya kuwasha pamoja na kupigwa kwa waandamanaji na kumshika mwenyekiti huyo Halima Mdee pamoja na wafuasi wake na kupelekwa polisi Osterbay leo.
Polisi wakimpandisha Halima mdee kwenye gari la polisi leo
Halima Mdee akiwa ndani ya gari la polisi pamoja na wafuasi wa chadema wakipelekwa katika kituo cha polisi cha Osterbay.
Halima mdee akizozana na polisi mara baada ya kuingizwa kwenye gari
Wafuasi wa chadema wakimueleza polisi madai yao wakiwa nje ya kituo cha polisi cha Osterbay wakidai kwenda kwa wanaohusika kutuoni hapo kwa ajili ya kumtoa mwenyekiti wao Halima Mndee
Wafuasi wa chadema wakilalamika kwa polisi
Kituo cha polisi cha Osterbay kilikuwa na ulinzi wa kutosha na hakuruhusiwa mtu yeyote kuingia kituoni hapo
Polisi wa Osterbay wakizuia gari kupitia
Wakina mama wa chadema wakifika katika eneo la polisi Osterbay
Viongozi wa chadema wakiomba kuruhusiwa kupita polisi ya Osterbay
4 comments:
ccm oyee na ma ccm wote huko majuu marekani na uingereza oyeee.
democracy at work ya ccm
CHAMA CHA SIASA ni MABARABARANI NA MAJUKWAANI - JK NYERERE .
salama jabir naye alikuwepo katika maandamano kumsupport Halima mdee?
Kitendo cha polisi kuwapiga wanawake, hasa Halima mdee, ni kitendo cha aibu na kinatakiwa kilaaniwe na Watanzania wote wenye akili timamu. Wanawake wote bila kujali wewe ni CCM, CUF, NSSR mageuzi ni lazima mtoe tamko kwa wanawake wenzenu kudhalilishwa kiasi hiki. Wanawake kwa asili yao kimaumbile si watu wenye nguvu sana, inasikitisha kuona polisi wanaume wanampiga Halima Mdee kwa virungu utadhani wanakamata jambazi. Kitendo hiki kimenipa huzuni sana, ingawa kuandamana ni haki ya watanzania lakini kuwapiga wanawake virungu ni aibu. Nchi zingine watu wanaandamana lakini polisi wanawakamata kwa kwa ustaarabu, si kama ilivyotokea leo. Wito wangu, wanawake wote, watanzania wote bila kujali tofauti zetu tulaani kitendo hiki cha kihuni.
Post a Comment