Advertisements

Thursday, October 23, 2014

AU YAWATUNUKU DKT. SALIM NA BALOZI MBITA TUZO ZA JUU ZA MWANA WA AFRIKA


Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim akipokea Tuzo ya Juu ya Umoja wa Afrika ya Mwana wa Afrika kwa Mwaka 2014 kutoka kwa Kamishna wa Amani na Usalama wa Umoja wa Afrika, Mhe. Balozi Smail Chergui. Tuzo hiyo ilitolewa mjini Arusha pembezoni mwa Warsha ya Tano ya Ngazi ya Juu kuhusu Amani na Usalama Bararani Afrika iliyoandaliwa na Umoja wa Afrika inayoendelea mjini humo. Tuzo hiyo pia imetolewa kwa Balozi Mstaafu na Mpigania Uhuru Mahiri Barani Afrika, Balozi Hashim Mbita. Tuzo hizo zimetolewa kwao kutokana na mchango mkubwa walioutoa Barani Afrika na kwa Umoja wa Afrika ambapo Dkt. Salim alikuwa Katibu Mkuu wa saba wa OAU kuanzia mwaka 1989 hadi 2001. Kwa upande wake Balozi Mbita alikuwa Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Ukombozi Barani Afrika chini ya OAU kuanzia mwaka 1974 hadi 1994 ilipomaliza kazi yake baada ya Uhuru wa Afrika Kusini. 
Balozi Chergui akimkabidhi Cheti cha Tuzo hiyo Dkt. Salim 
Dkt. Salim akipongezwa na Balozi Chergui 
Balozi Chergui akimkabidhi Tuzo ya Juu ya Umoja wa Afrika ya Mwana wa Afrika ya Mwaka 2014, Binti wa Balozi Hashim Mbita, Sheila Hashima Mbita ambaye aliipokea Tuzo hiyo kwa niaba ya Baba yake ambaye hakuweza kufika kutokana na matatizo ya kiafya. 
Balozi Chergui akimkabidhi Cheti Bi. Sheila Hashim Mbita kwa niaba ya Balozi Mbita
kwa picha zaidi bofya soma zaidi 
Balozi Chergui akimpongeza Bi. Sheila Hashim Mbitaaliyepokea Tuzo kwa kwa niaba ya Balozi Mbita 
Ujumbe wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwemo Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Balozi Naimi Aziz wakipiga picha ya pamoja na Dkt. Salim Ahmed Salim na Bi. Sheila Hashim Mbita mara baada ya kukabidhiwa Tuzo hizo. 
Dkt. Salim akipongezwa na Balozi Augustine Mahiga huku Rais Mstaafu wa Cape Verde (kulia) akushuhudia. 
Dkt. Salim akipongezwa na wajumbe mbalimbali waliokuwepo wakati wa hafala ya utoaji Tuzo. 
Dkt. Salim katika picha ya pamoja na Balozi Naimi Aziz 
Dkt. Salim katika picha ya pamoja na Bi. Zuhura Bundala, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. 
Balozi Aziz katika picha ya pamoja na Bi. Sheila Mbita 
Balozi Aziz akiwa na Balozi Mahiga katika picha ya pamoja na Bi. Sheila Mbita.

No comments: