Advertisements

Thursday, October 2, 2014

CHA MPENZI WAKO CHAKO, CHAKO CHAKO, HOW COME?


Ni wiki nyingine tafauti kabisa na wiki zilizopita tunakutana tena kupitia safu hii namba moja kwa kuandika makala ‘hot’ za mapenzi. Ni safu ambayo inaweza kuyafanya maisha yako ya kimapenzi yakawa ya furaha endapo tu utayafanyia kazi yale ambayo huwa nayaandika.

Kikubwa unachotakiwa kujua ni kwamba, ukikosea kidogo tu kwenye mapenzi huwezi kuwa na furaha kwenye maisha yako. Unaweza kwa na pesa nyingi benki, mali kibao lakini kama mapenzi yanakuzingua, utakosa amani na wakati mwingine kuhisi huna thamani ya kuendelea kuishi.

Waliojiua kwa sababu ya mapenzi wapo, waliochanganyikiwa na kushindwa kufanya kazi zao kwa ufasaha ni wengi sana. Hivyo basi, ili uwe na maisha yenye amani na utulivu, tumia gharama yoyote kujihakikisha maisha ya amani ya kimapenzi ikiwa ni pamoja na kuchagua mwenza sahihi.

Mpenzi msomaji wangu, leo nataka kuzungumzia hili suala la baadhi ya watu kuwa wabinafsi, wabahili na wasiowajali wapenzi wao na kusababisha mapenzi yao kuwa dhaifu.

Nilishawahi kuzungumzia suala la baadhi ya wanaume kuwa wabahili kwa wapenzi wao. Yaani wao kutoa pesa zao kuwafanyia ‘shopping’ wapenzi wao, kuwasaidia pale wanapokuwa na matatizo ni wagumu kuliko maelezo.

Unakuta mwanaume anapata mshahara mzuri au katika mishemishe zake anakuwa na bahati ya kupata mshiko wa kutosha lakini ukifuatilia sana utabaini ni mgumu kutoa na mpenzi wake hanufaiki chochote na kipato hicho kizuri.

Akiombwa pesa ya vocha anakuwa mkali sana, akililiwa shida anaweza hata kukata mawasiliano kwa kuhisi eti akitoa pesa yake ataonekana kachunwa. Jamani, labda niseme kwamba, mpenzi wako anayekupenda kwa dhati hawezi kukuchuna. Anapokulilia shida, anajua wewe ndiye mtu sahihi wa kumsaidia. Hawezi kwenda kwa mtu wa pembeni na kuomba msaada wakati wewe upo.

Hivi mpenzi wako akimlilia shida rafiki yako (shemeji yake) na akapewa wakati wewe ulikuwa unaweza kumsaidia utajisikiaje? Mpenzi wako akiwa anavaa midabwada, anaishi kwa kuungaunga wakati wewe mambo yako safi hujisikii vibaya? Usipokuwa wa kwanza kumfanya mpenzi wako ajisikie furaha kwenye maisha yake, unatarajia nani afanye hivyo?

Sikatai huenda kazi huna na fedha inakupitia kushoto, hilo wala siyo tatizo. Kwa kuwa mpenzi wako anajua naamini ataendelea kuwa na wewe akifahamu kuwa kukosa kwako ni mipango ya Mungu. Tatizo ni pale ambapo unazo na unakuwa bahili bila sababu za msingi. Huku ni kutaka kumfanya mpenzi wako ashawishike kuchepuka.

Atakutana na wanaume wanaoujua kumwaga pesa na wenye ushawishi mkubwa na kwa kuwa wewe humjali, atajikuta amechepuka. Tusitake yatukute hayo!Lakini sasa wakati hilo likiwa hivyo, leo nataka kuwazungumzia baadhi ya wanawake ambao wana katabia f’lani kasikofaa. Nawazungumzia wale wanaofanya kazi zinazowaingizia kipato, hata kama siyo kikubwa kuzidi kile cha waume zao.

Ni kweli mume ana jukumu la kumfanya mkewe ajikisikie furaha ya kuolewa lakini wewe mwanamke ambaye unapata pesa kwa kazi zako au mshahara, ni lini ulisema leo ngoja nimsaidie mpenzi wangu katika hili?

Yaani kwa kuwa umeolewa basi unataka kila kitu mumeo afanye, yeye ndiye anunue chakula, atoe mahitaji muhimu kwa watoto, akuvishe na akulishe, fedha zako wewe unafanyia nini?

Ni lini ulisema leo ngoja ninunue mahitaji ya nyumbani? Ni lini ulimnunulia zawadi mpenzi wako? Mara ya mwisho ni lini kumtumia mumeo vocha? Wewe jifanyie tathmini kisha majibu yako uyawekee vingi viulizo.

Nasema hivyo kwa kuwa, wapo wanawake ambao wanaamini kipato chao wana haki ya kukifanyia chochote ila cha mume ndicho kinachotakiwa kutumika ipasavyo.

Wapo wanawake ambao wako makini sana na mshahara wa waume zao lakini za kwao wakiulizwa wanakuwa wakali, hii siyo sawa!Mnapokuwa wapenzi au mmeoana, mnakuwa kitu kimoja. Mwenzako akiwa na shida f’lani unamsaidia pale inapobidi lakini itakuwa haileti picha nzuri kama pesa yako ni yako lakini ya mpenzi wako unaitolea macho.

Ninachotaka kusema hapa ni kwamba, kama kweli unampenda huyo uliyenaye, usijenge utegemezi uliopitiliza. Usiwe ni mtu wa kila siku kutaka usaidiwe, wakati mwingine umsaidie mwenzako pale ambapo unaona una uwezo na yeye ana shida.

GPL

No comments: