Facebook imewachukulia hatua wanaouza Likes kwenye Facebook
Mtandao wa kijamii wa Facebook umeahidi kujitahidi kukabiliana na uuzaji na ununuzi wa 'Likes' bandia kwenye mtandao huo.
Facebook inasema imeshinda dola bilioni mbili katika kesi iliyowasilisha mahakamani dhidi ya watu wanaouza 'Likes' za bandia kwa wafanyabiashara walio na akaunti kwenye mtandao huo.
Inaarifiwa wamiliki wa makampuni wananunua 'Likes' kwenye mtandao huo ili akuanti zao kuonekana kuwa maarufu na kupendwa na watu wengine wakati sio kweli.
Lakini Facebook imesema kuwa wanunuzi wa 'Likes' kwa njia za kimagendo wanafanya jambo baya kwa wafanyabiashara wengine na ina maana kuwa kampuni nyinginezo zenye akaunti zao kwa Facebook heunda zikapata hasara.
Katika taarifa yake, Facebook iliandika na kusema: 'Tunataka kuhakikisha tunakomesha tabia ya ununzzi wa 'Likes' kwa sababu wenye biashara na watu wa kawaida wanataka kuwasiliana kwa lengo la kupata mafanikio sio mambo bandia. ''
Mtandao huo ulielezea kuwa wauzaji wa Likes bandia wanawapa 'admins' au wasimamizi wa akaunti fulani fursa ya kununua 'Likes' kama 10,000 bandia ili watu wapende akaunti zao.
Kwa sababu sakata kama hizi zinalenga zaidi kufaidika kifedha na hasa kuwahadaa wafanyabiashara , tunalenga kuwakomesha watu kama hao.
Mtandao huo umesema mbali na kuchukua hatua za kisheria pia unalenga kutumia teknolojia mpya ya kubana uuzaji na utengezaji wa Likes bandia.
No comments:
Post a Comment