Akiwa mmoja kati ya wanadada wanofanya vizuri sana kwenye Tasnia hii ya Bongo Movies ,Wema Sepetu ni msichana anayetoka kwenye Familia ya kibalozi ni mtoto wa mwisho katika familia ya wasichana wanne wa Balozi Isaack Sepetu Ibrahimu.
Ana sura na umbo zuri sana, na mvuto mkubwa sana kutokana na rangi yake nzuri ya ngozi. Wema sepetu alizaliwa mnamo mwaka 1988 katika hospitali ya ST. Andrew’s jijini Dar es Salaam na ni mtoto wa mwisho kuzaliwa katika familia yao yenye watoto wanne wa kike.

Pamoja na kuwa na kipaji cha uigizaji wema pia anakipaji kikubwa cha kuimba na pia alishawahi kushiriki mashindano ya urembo na kufanikiwa kutwaa taji la Miss Tanzania mnamo mwaka 2006 na kujipatia zawadi ya gari aina ya Toyota Rav 4.
Credit:Bongoclan
No comments:
Post a Comment