Mbunge wa Kawe na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha),Halima Mdee.
Baada ya kukamatwa akifanya maandamano yenye nia kwenda Ikulu kumshinikiza Rais Kikwete kutoipokea Rasimu ya Katiba inayopendekezwa, Mbunge wa Kawe na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha), Halima Mdee, anatarajiwa kuripoti leo katika Kituo cha Polisi Oysterbay, jijini Datr es Salaam.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camillius Wambura, alisema kuwa mbunge huyo ataripoti kituoni hapo ili kufahamu hatua zingine za kisheria zinazoweza kuchukuliwa dhidi yake na wenzake tisa.
“Anatakiwa kuripoti kesho (leo) kutokana na maandamano waliyoyafanya, akisharipoti tarartibu zingine zitajulikana mara tu baaada ya kupokea jalada kutoka kwa Wakili wa Serikali,” alisema Wambura.
“Aliaachiwa juzi (Jumamosi) baada ya kutimiza masharti ya dhamana, jalada likishafika itajulikana hatua gani itakayoendelea dhidi ya Mdee,” aliongeza.
Wengine waliokamatwa ni Martha Charles, Beauty Mmari, Anna Linjewele, Sofia Phanuel, Remina Peter na Mwanne Kassim. Hata hivyo, siku hiyo jioni kwa dhamana baada ya kutimiza masharti.
NIPASHE ilifanya jitihada za kumatafuta mbunge huyo kupitia simu yake ya mkononi, lakini hakupatikana.
Mdee pamoja na wanachama wengine wa Chadema Oktoba 4 mwaka huu, walikamatwa katika maandamano yaliyokuwa na lengo la kwenda kuonana na Rais Jakaya Kikwete kumshawishi kutoipokea Rasimu ya Katiba inayopendekezwa, ambayo ilipitishwa na Bunge Maalum la Katiba Alhamisi iliyopita.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment