ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, October 7, 2014

Ugonjwa mpya waibuka Mtwara

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dk. Seif Rashid.

Ugonjwa uliodhaniwa kuwa ni surua, ulioibuka katika shule ya Msingi Mkoma1, Kata ya Mnikachi wilaya ya Newala, Mtwara, imebainika siyo surua baada ya sampuli zilizochunguzwa kuonesha kuwa ugonjwa huo ni rubella.

Dalili za ugonjwa huo zinazodaiwa kuwa sawa na ugonjwa wa surua zimeelezwa kuwa ni pamoja na kuwashwa macho, homa, kuharisha, ngozi kuwasha, vipele, kubabuka midomo, mafua, kuumwa tumbo, ngozi kukakamaa pamoja na kupoteza hamu ya kula.

Watu wapatao 552 wanadaiwa kuambukizwa tangu kuwepo kwa ugonjwa huo.Katika shule ya Msingi Mkoma 1, wanafunzi 45, wamegundulika kuwa na maambukizi mapya huku 32 na mwalimu mmoja wa Afya, Mwanahamaisi Madidi, wakiugua tena maradhi hayo.


Ugonjwa huo ambao awali ulikuwa ulidaiwa kuwaambukiza wanafunzi na watoto, lakini kwa sasa unawakumba watu wazima.Vijiji vilivyoathiriwa ni Mkoma 1, Imani, Mitahu Mnauke Nakahako na Chiwambo.

Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Mkoma 1, Awadhi Mkanapate, alisema tangu Agosti mwaka huu ulipolipuka, wanafunzi 368 waliugua sambamaba na walimu watano.

“Hali ya sasa ni tofauti kidogo na hali ya awali, lakini jambo la kushangaza ugonjwa huu unawarudia hata wale walioumwa mara ya kwanza, mara ya kwanza wanafunzi 368 na walimu watano waliumwa ugonjwa huu, lakini mpaka sasa wanafunzi 323 wamepona,” alisema.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mitahu, Chipila Ajali, alilieleza NIPASHE kuwa ugonjwa huo uliibuka shuleni hapo mwezi uliopita.“Kabla hatujafunga shule hatukuwa na maambukizi ya ugonjwa huu isipokuwa kwa wenzetu wa shule ya Mkoma 1, lakini baada ya kufungua shule mpaka sasa tuna idadi ya wanafunzi 12
Abdallah Lilanga (70), Mwenyekiti wa kijiji bodi Zahanati ya Mkoma 1, alisema:

Mwenyekiti wa kijiji hicho, Athuman Rajabu, alisema wamechukua hatua za kudhibiti ugonjwa kwa kuzuia, upikaji na uuzaji wa pombe za kienyeji na kucheza ngoma.

“Awali wakati maambukizi yanaanza tulizuia mikusanyika, lakini baada ya kupungua ugonjwa huu wananchi wameanza mikusanyiko tena, na vijiji jirani wanakuja hapa kunywa pombe ndiyo maana maambukizi yanazidi kuenea mpaka vijiji jirani,” alisema Rajabu.

Muuguzi wa zamu zahanati ya Mkoma 1, Thomas Kilatu, alisema maambukizi yanazii kuongezeka, kutokana na kutokuwepo kwa dawa maalum ya kutibu ugonjwa huo.

“Mwanzoni tulizani ni surua, lakini baada ya sampuli kurudi inaonekuwa kuwa siyo surua bali ni rubella ambao una dalili sawa na surua,” alisema.

“Tupo katika hatari ya kupata maambukizi, hatujui kama na sisi tutapata ugonjwa huu hali itakuwaje,” alisema.

Alisema Oktoba 18, mwaka huu ni siku ya kampeni ya kutoa chanjo ya surua nchi nzima, lakini kutokana na sampuli hizo kuonyesha kuwa ugonjwa huo siyo surua hawajui la kufanya.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Newala Dk, Yudas Ndungile, alisema mpango wa utoaji chanjo upo pale pale na kwamba tayari vifaa vimekwisha sambazwa.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments: