Washiriki wa mkutano mkuu wa mwisho wa mwaka uliowahusisha wakuu wa TEHAMA wa sekta mbali mbali nchini Kenya wakiendelea na Mkutano wao jijini Nairobi kujadili mambo mbalimbali na changamoto zake.
Kushirikiana katika maswala mbali mbali ili kuweza kufikia malengo ni jambo kubwa lililopata kusikika katika mkutano mkuu wa mwisho wa mwaka unaoendelea nchini Kenya unaojadili changamoto mbali mbali za sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
Swala la usalama katika mitandao limepata kuangaliwa na changamoto mbali mbali katika mijadala Rasmi (Ndani ya Kikao) na isiyo rasmi (tuwapo nje ya ukumbi wa mkutano) zilipata kuangaliwa kwa ukaribu.
Swala uhimu nililo jifunza ni jinsi uhalifu mtandao katika mataifa haya mawili Kenya na Tanzania yanavyofanyika na kujua ya kuwa kubadilishana mawazo katika hili litasaidia kujipanga kukabiliana na uhalifu mtandao ambao tayari kwa nchi ya Kenya umeendelea kukua.
Ikiwa bado kwa Tanzania haujaonekana sana huku Kenya nilijifunza pia ili kuweza kujipanga kabla ya uhalifu usika kuweza kushika kasi.
Namna mbalimbali zinazotumika na wenzetu wa Kenya ambao wameathirika sana na uhalifu mtandao (Mfano: Wakati Mkutano unaendelea – Baadhi ya mifumo mtandao ya serikali iliripotiwa kuangushwa na wahalifu mtandao) kwenye kukabiliana na uhalifu mtandao huku tukiangalia kwa karibu namna ambavyo teknolojia zinazotumika kupambana na uhalifu mtandao katika nchi hiyo zinavyoweza kutoa msaada wa kina kwenye makabiliano na uhalifu mtandao Nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment