Friday, October 3, 2014

Mgosi: Jaja akizoea Bongo atakuwa hatari

Straika wa Yanga, Mbrazili, Geilson Santana ‘Jaja’.

Na Alpha Amos 
STRAIKA wa Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro, Mussa Hassan Mgosi, amemtabiria makubwa straika wa Yanga, Mbrazili, Geilson Santana ‘Jaja’ kwa kusema atakuwa mchezaji mzuri pindi atakapozoea mazingira ya Tanzania na viwanja nyake.
Jumamosi iliyopita, Mgosi aliifungia timu yake bao moja katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Yanga, huku Jaja akishindwa kufunga na kukosa penalti.
Mshambuliaji wa Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro, Mussa Hassan Mgosi.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Mgosi alisema Jaja ni mchezaji mzuri ila bado hajazoea mazingira ya viwanja vya Tanzania, ndiyo maana anapata wakati mgumu.
“Jaja ni mchezaji mzuri sana ili bado hajazoea mazingira ya Tanzania, hivyo kumfanya ashindwe kufanya vizuri ila atakuwa mzuri zaidi baada ya kuzoea mazingira. Anahitaji kuzoea mazingira ya viwanja vyetu vya Tanzania ndipo aweze kufanya vizuri,” alisema Mgosi.

No comments: